loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba, Yanga zabanwa mikoani

TIMU za Simba, Yanga na Mtibwa Sugar jana jioni zilijikuta zikibanwa ugenini baada ya kulazimisha sare kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa kwenye viwanja tofauti.

Mabingwa wa tetezi wa Ligi hiyo, Simba walikuwa wanakabiliana dhidi ya Ndanda mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, wakati Yanga walipambana na Biashara United kwenye dimba la Karume Mara na Mtibwa Sugar walifungana bao 1-1 mbele ya Alliance FC.

Matokeo hayo yanawafanya vinara Simba kufikisha pointi 80, Yanga wanafikisha pointi 61 wakibakia nafasi ya pili, hivyo huenda ikawa kwa muda, kwani Azam FC nao jana jioni walitarajiwa kushuka uwanjani kumenyana na vibonde wa ligi hiyo, Singida United.

Ushindi wa pointi tatu kwa Azam wenye pointi 59 kama watashinda kwenye mchezo huo, basi huanda wakabadili msimamo wa ligi hiyo kwa kupanda nafasi ya pili, kwani wanatofautiana na Yanga kwa pointi mbili tu.

Pia, sare hiyo haijawanufaisha Ndanda kwani wamefikikisha pointi 36 wakisalia nafasi ya 17, wakati Biashara wakibaki nafasi ya tisa wakifikisha pointi 45 wote wakicheza michezo 33 na Mtibwa wanakalia nafasi ya 14 kwa jumla ya alama 38 na Alliance wenye alama 37 nafasi ya 16.

Mechi kati ya Yanga dhidi ya Biashara ilianza kwa kasi kwa mabingwa hao wa kihistoria mara 27 wakitawala mchezo kwa kulisakama lango la wapinzani wao mara kwa mara, lakini hata hivyo umakini wa safu ya ulinzi ulisaidia kuondoa hatari zote zilizokuwa zinatokea.

Hadi timu hizo zinaenda mapumziko, milango ilikuwa migumu kwa pande zote.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ya wachezaji wakiwa na dhamira ya kubadilisha mchezo na kupata mabao, lakini wenyeji Biashara waliokuwa na malengo mawili kwenye mechi hiyo kushinda hama kutoka sare, walionekana kuwa bora zaidi kwa kumiliki mpira.

Wakati Yanga wanacheza kwa kijilinda na kufanya mashambulizi ya kushtukiza hadi pambano linakamilika ndani ya dakika 90, akuna timu iliyoruhusu nyavu zake kutikiswa.

Kwa upande wa Simba, wenyewe walishambuliana kwa zamu na Ndanda FC, lakini hakuna upande uliobahatika kuibuka na ushindi.

Kabla ya kuanza kwa mchezo, Simba ambao Jumatano iliyopita walitetea ubingwa wao baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons na kufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoye, waliandaliwa gwaride la heshima na wenyeji wao mjini Mtwara ikiwa heshima ya kutwaa taji hilo.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi