loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Tunawajua Simba, tutawamaliza'

NAHODHA wa Yanga, Juma Abdul, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwataka kuwa na furaha kwenye kipindi hiki ambacho wanafanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Yanga watacheza dhidi ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation (FA), utakaofanyika Jumamosi ya mwishonimwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Abdul alisema timu hiyo inaendelea kujipanga kikamilifu kuwakabili Simba na kuwataka mashabiki wa Yanga waache kuwasikiliza wapinzani wao, kwani mbinu wanazopewa kwa sasa zinalenga kwenda kupata ushindi.

“Mashabiki wa Simba wanaongea kiasi kwamba mashabiki wetu wameanza kurudi nyuma, niwaombe waendelee kuwa na furaha kwenye kipindi hiki kwani ubora wa kikosi cha Simba tunaujua na mbinu anazotupa mwalimu zinalenga kwenda kumaliza mchezo ndani ya dakika 90,” alisema Abdul.

Alisema ndani ya msimu huu watakutana mara ya tatu na wapinzani wao hao na wamefanikiwa kuchukua pointi nne, baada ta kutoka sare mara moja na kushinda mara moja kabla ya kukutana tena Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa nusu fainali ya FA.

Alisema malengo yao kama timu, wataingia kwenye mchezo huo wakiwa kwenye harakati ya kutafuta tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa kupitia Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga kwa sasa wanatolea macho Kombe la FA kama njia ya pekee ya kutafuta tiketi kuiwakilisha nchi kimataifa baada ya kupoteza muelekeo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambako Simba tayari wametetea ubingwa wao kwa mara ya tatu mfululizo.

TIMU ya soka ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi