loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tandahimba City yafuzu Nane Bora

TIMU ya Tandahimba City ya Mtwara imefuzu kucheza Nane Bora, baada ya kuifunga Livingstone ya Njombe kwa mabao 2-0, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa mikoa, uliochezwa juzi Uwanja wa CCM Tunduru.

Katika mchezo huo wa Kundi D Kituo cha Tunduru, mkoani Ruvuma, Tandahimba walipata bao la kwanza dakika ya 13 lililofungwa na Nasri Seleman baada ya kutokea piga nikupige katika goli la Livingstone FC.

Katika kuonesha kama wamepania kushinda, dakika ya 29, Yasin Hamis, alifunga bao la pili kwa shuti la mbali na kuifanya Tandahimba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 2-0.

Kwa matokeo hayo, Tandahimba imeungana na Korosho kufuzu kucheza nane bora, ambayo itafanyika kuanzia Julai 10 kwenye kituo ambacho kitangazwa hapo baadaye. Katika Kundi A lililopo Kigoma, Kiluvya FC na Kibondo Youngstar nazo zimefuzu Nane Bora.

Kundi B lililopo mkoani Kilimanjaro, Muheza United inaongoza ikiwa na pointi 10, ikifuatiwa na Nyamongo yenye pointi nane, Cable Stars ina pointi sita na jana ilitarajiwa kucheza mchezo wa mwisho na ikishinda itaungana na Muheza kufuzu nane bora, maana itaizidi Nyamongo kwa pointi mbili.

Katika Kundi C lililopo Gairo, Morogoro, Nyika FC imejihakikishia nafasi ya kucheza Nane Bora na endapo 515 KJ itashinda itaungana na Nyika ila kama ikifungwa, basi Kurugenzi FC itafuzu.

Mashindano hayo ambayo yalianza Juni 25 baada ya kusimama kutokana na janga la corona, yalitarajiwa kumalizika jana.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo, Tunduru

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi