loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Utatu Man United usipime

WAKATI Manchester United ilipomuuza Romelu Lukaku kwa Inter Milan katika kipindi kilichopita cha majira ya joto, walilaumiwa sana kuwa wamefanya kosa kubwa kwa kuiacha timu hiyo bila mbadala katika ufungaji mabao.

Wakati kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kiliposhinda mechi mbili tu kati ya saba mwanzoni mwa mwaka 2020 na kuwa na pointi sita nje ya nne bora, ilishangaza walipomsajili kwa mkopo Odion Ighalo kutoka klabu ya Ligi Kuu ya China na kufanya wengi kuhoji uamuzi huo.

Lakini baada ya United mwaka huu kuimarika zaidi kutokana na utatu wa washambuliaji wake, ambao Jumamosi waliiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Washambuliaji wake, Anthony Martial, Marcus Rashford na Mason Greenwood, ndio walikuwa mashine ya kutengenezea mabao hayo, huku wakifunga jumla ya mabao 55, kati yake katika mashindano yote msimu huu.

Walifunga mabao manne walipocheza dhidi ya AFC Bournemouth, ambayo inajulikana pia kama Cherries, huku mawili yakifungwa na Greenwood na Rashford na Martial kila mmoja akipachika moja.

Hii ni mara ya tatu tangu Krismasi iliyopita wote kufunga katika mechi ya Ligi Kuu, huku mmoja kati yao akifunga mara mbili katika kila tukio.

Katika kudhihirisha makali ya safu hiyo ya ushambuliaji, United imefunga mabao matano au zaidi katika matukio manne katika mechi 16 zilizopita. Walifanya hivyo mara tatu katika mechi za kwanza 367 baada ya kustaafu kwa kocha Sir Alex Ferguson.

“Jinsi gani unavutiwa naye?,” aliuliza mshambuliaji wa zamani wa England Ian Wright alipozungumza na BBC baada ya Green- wood kufunga mabao mawili.

Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solsk- jaer, alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 huenda akawa mmaliziaji mzuri golini, ambaye hajawahi kutokea.

Kwa sasa United wako na pointi mbili nyuma ya Chelsea katika mbio za kuwania nne bora, lakini wenyewe wako nafasi ya tano ambayo itatosha kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, endapo kifungo cha Man City kucheza Ulaya kitaendelea. Pia bado wapo katika mashindano ya Ligi ya Ulaya pamoja na Kombe la FA.

WAKALI WATATU

Wengi wanajiuliza jinsi gani wakali hao watatu wanavyoliganishwa Ulaya. Watatu hao wa Man United wamefunga mabao mengi katika mashindano yote msimu huu kuliko wakali wa Liverpool, Mohamed Salah (21), Sadio Mane (19) na Roberto Firmino (11).

Ni timu sita tu Ulaya, ambazo zina wachezaji watatu waliofunga mabao 55, ukichanganya pamoja yaliyofungwa na Rashford, Martial na Greenwood.

Mfano wachezaji watatu wanaoongoza kwa mabao Bayern Munich, ambao wamefunga kwa pamoja jumla ya mabao 83, ambao ni Robert Lewandowski alifunga 51, Serge Gnabry 20 na Thomas Muller 12. Kwa upande wa Paris St-Germain, wafungaji wakali watatu, ambao kiujumla wamefunga mabao 68 (Kylian Mbappe 30, Mauro Icardi 20 na Neymar 18).

Wakali watatu kwa Manchester City kwa ujumla wamefunga mabao 64, ambao sio wakati wote wamekuwa wakicheza pamoja. Sergio Aguero na Raheem Sterling kila mmoja ana mabao 23, huku 18 yakifungwa na Gabriel Jesus.

Wakali watatu wa RB Leipzig, wenyewe wana mabao 60, huku Chelsea ikifunga 34, ambao ni Timo Werner alifunga nane, 16 alifunga Marcel Sabitzer na 10 alipachika Emil Forsberg. Lionel Messi (27), Luis Suarez (16) na Antoine Griezmann (14), wamefunga jumla ya mabao 57 kwa Barcelona.

Lakini wanaofuatia ni wakali hao watatu wa Man United, wakiwa sawa na watatu wa Juventus, Cristiano Ronaldo (29), Paulo Dybala (17) na Gonzalo Higuain (9). Wako mbele ya wengi, wakiwemo wafungaji wa Liverpool (51) na Borussia Dortmund ambao wamefunga 48 (Jadon Sancho, Erling Braut Haaland na Marco Reus).

Lukaku amefunga mabao 25 kwa Inter Milan msimu huu ambao unamfanya kuwa mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi, lakini wafungaji wawili wa mabao mengi wanaofuatia kwa ujumla wamefunga mabao 22 tu.

Atalanta (52) na Lazio (48) ni miongoni mwa timu nyingine zenye wafungaji wazuri, lakini haziwezi kuwafikia watatu hao wa United.

Wakali watatu wa Real Madrid kiujumla wamefunga mabao 38 tu, huku Karim Benzema (22) na Sergio Ramos (11).

Ikiwa washambuliaji hao watatu wa United wataendeleza makali yao, basi klabu hiyo haina haja ya kusajili mshambuliaji mwingine wa kwanza katika kipindi hiki, licha ya kuwapo tetesi kuwa wanataka kufanya hivyo.

Kwa sasa, Greenwood ana umri wa miaka 18, wakati Rashford ndio kwanza ana miaka 22. Martial katika kundi hilo na mkongwe wao, kwani sasa ana miaka 24.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi