loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ali Kiba amtimua meneja

MSANII wa kizazi kipya, Ali Kiba, amesema kutokuelewana na meneja wake ni miongoni mwa sababu iliyochangia amuachishe kazi kwenye kampuni yake ya King Kiba.

Ali Kiba ambaye ni Rais wa lebo ya King Kiba, amethibitisha kufanya hivyo na kueleza kwamba, malengo yake kama kampuni ni kufanya kazi kwa kufuata maadili ili kampuni ifikie maendeleo endelevu.

“Ni kweli sifanyi naye kazi tena. Ni taratibu za kazi, amekuwa na mchango kwenye kampuni yetu katika kipindi cha nyuma, lakini kuna vitu vilitokea na tukawa hatuelewani, kama uongozi tukakubaliana tumuondoe. Lakini sio kwamba hawezi kazi,” alisema.

Msanii huyo alisema kuondoka kwa meneja huyo hakutakuwa na hasara kwenye kampuni hiyo, kwani kuna mwingine aliyekuwa anaandaliwa kuziba nafasi hiyo.

Wiki iliyopita, kampuni hiyo ilimtimua kazi meneja wake wa kike, Esi na nafasi yake inatarajiwa kushikiliwa na mmoja kati ya viongozi wa kampuni hiyo.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi