loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bil 28/- kujenga vituo 5 vya gesi asilia

UJENZI wa vituo vikubwa vitano vya kujazia nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kwenye magari, unatarajiwa kukamilika Juni mwakani baada ya kutengwa kwa Sh bilioni 28 za ujenzi. Ujenzi huo unafanyika baada ya watu wengi kuanza kutumia nishati hiyo kuendesha magari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania(TPDC), James Mataragio alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLEO kuhusu matumizi ya gesi asilia.

Mataragio alisema kabla ya hapo, kulikuwa na kituo kimoja cha kujazia gesi Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam hivyo mwaka wa fedha 2019/2020 zilitengwa fedha hizo kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa vituo hivyo vingine.

“Tutaanza na vituo hivi vikubwa vitano, kisha tumeitisha zabuni kujenga vituo vingi vidogo vidogo na watu 24 wameonesha nia,”alisema.

Alisema vituo vikubwa vitajengwa Kivukoni, Maliasili(barabara ya Nyerere), Kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Barabara ya Nelson Mandela na Kibaha katika mkoa wa Pwani.

Alisema mpaka sasa tayari amepatikana mkandarasi na ameshaanza kuchora michoro ya ujenzi kilichochelewesha ni mlipuko wa ugonjwa wa maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema utumiaji wa gesi asilia kwenye magari ni nafuu asilimia 40 ya utumiaji wa nishati nyinginezo na gesi asilia haichafui mazingira.

“Kilo moja ya gesi ni Sh 1,500, bei ya mafuta kwa ujazo huo ni Sh 3,500 na mafuta hayo hayo magari yatakwenda umbali sawa sawa,”alisema.

Taarifa katika mtandao wa TPDC zinaonesha matumizi ya gesi asilia katika magari nchini yamekua ambapo hadi Agosti 2019, watu 210 kutoka 65 wa mwaka 2017 na sasa ni 400.

Agosti 21, 2019 akiwasilisha taarifa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu hatua zilizofikiwa kuandaa moduli ya miradi ya bei ya gesi asilia, uuzaji, usambazaji majumbani na viwandani, Dk Mataragio alisema kutokana na ongezeko hilo, kituo cha majaribio Ubungo Dar es Salaam, kinashindwa kuhimili matakwa ya matumizi hivyo shirika lilijipanga kujenga kituo kikubwa eneo la Sam Nujoma jijini humo.

“Kituo hicho kinachotarajiwa kukamilika Oktoba 2020, kitajaza gesi katika magari na kupeleka gesi maeneo mabomba ya gesi bado hayajafika, maeneo ya viwanda Kigamboni na Kibaha, Feri na pia huko Muhimbili,”alisema.

Alisema huo ni mwendelezo wa jitihada za uwezeshaji matumizi ya gesi katika magari. Alisema TPDC inalenga kuupatia gesi asilia mradi wa mabasi ya mwendokasi (DART).

Alisema kwa kuanzia, kituo cha kujazia gesi magari kitajengwa DART, depoti ya Ubungo na kinatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Alisema shirika limekubaliana na DART kuwezesha kuweka vituo maalumu vya gesi katika depoti ya Gongo la Mboto na Mbagala ili kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi ya DART na kuongeza matumizi ya gesi asilia.

Alisema gesi asilia ni nishati safi inayovunwa nchini na ina unafuu mkubwa kuliko nishati nyingine hivyo wananchi wakitumia gesi serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Pia matumizi ya gesi asilia yanaokoa ukataji wa miti hivyo kila mtu akitumia gesi asilia itaokoa. Hadi Novemba 7, 2019, Tanzania ina akiba ya gesi futi za ujazo trilioni 57.54 huku matumizi ya rasilimali hiyo kwa sasa yakiwa kidogo na sehemu kubwa ikitumika kuzalisha umeme.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...