loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ileje, Nkasi wapewa miezi 3 vyuo vya ufundi

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezipa miezi mitatu Halmashauri za Wilaya ya Ileje mkoani Songwe na Nkasi mkoani Rukwa kuhakikisha wakazi wake wanatekeleza azma ya Serikali ya kujenga vyuo vya ufundi ili wanafunzi wakapate ujuzi.

Alisema iwapo wakazi wa halmashauri hizo hawatatekeleza agizo hilo na kutambua nia ya Serikali kuwapelekea vyuo vya ufundi, hatasita kuchukua hatua ikiwemo kufungua milango kwa vijana kutoka maeneo mengine nchini kwenda kunufaika na vyuo hivyo na kuwaaacha wenyeji wakivitazama kama mapambo tu.

Alisema hayo alipokagua na kuzindua vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Nkasi na Ileje ambapo hakuridhishwa na idadi ndogo ya wanafunzi waliojiunga na vyuo tangu vianze.

“Vyuo vya Veta ni vya Watanzania wote, lakini tunajenga kila Halmashauri wanufaika wa awali wawe vijana wa eneo husika kabla ya wale wa mbali kuja. Sasa nawapa miezi mitatu iwapo mtaendelea kutotumia fursa hii, tutachukua maamuzi mengine. Uzuri hapa yapo mabweni, tutachukua wanafunzi kutoka maeneo mengine waje kunufaika,”alisema Profesa Ndalichako.

“Lakini kwa nini msubiri watu watoke mbali wakati vijana wenu Ileje wanahitaji kupata ujuzi waweze kujiajiri na kuajiriwa? Ni wakati wenu kutafakari kuongeza idadi ya wanafunzi hapa ili pia msiwavunje moyo wadau waliopigania kuharakisha kuletwa kwa vyuo hivi kwenu.”

Aliwataka wakazi wa wilaya kunakojengwa vyuo vya Veta kujua nia ya serikali ni kupanua wigo wa vijana kuwa sehemu ya kushiriki jitihada za serikali za kuimarisha uchumi na ndiyo sababu inatumia fedha nyingi kujenga vyuo vipya na kukarabati vilivyokuwepo awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Veta, Peter Maduki alizitaka halmashauri za wilaya zilikoanzishwa vyuo vya ufundi na mikoa yake kuboresha mafunzo katika vyuo hivyo kwa kupeleka zabuni za kazi mbalimbali badala ya kupelekea mafundi wasio na mafunzo mitaani.

Alisema halmashauri ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zenye shughuli nyingi ambazo huhitaji sare, hivyo ni vyema wanapohitaji kushonewa wakapeleka zabuni hizo vyuoni ili wanafunzi wapate kazi na pia kuongeza ujuzi.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Ileje

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...