loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge atoa vifaa vya mil 10/- CCM

MBUNGE aliyemaliza muda Jimbo la Longido mkoani Arusha, Dk Stephen Kiruswa ametoa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 10 kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Longido.

Miongoni mwa vifaa hivyo vimo vitabu vikubwa 1,400, bendera, skafu na kalamu kwa ajili ya viongozi wa mashina (mabalozi) ili chama kijue idadi ya wanachama wake na pia wafanye kazi zao vizuri na kwa ubora zaidi.

Dk Kiruswa alisema amefanya hivyo baada ya kuona kuwa baadhi ya mabalozi hawajui majina ya watu wao wanaowaongoza, hawana namba zao za simu na chama wilaya kutokuwa na kanzidata ya wanachama jambo ambalo si sawa.

Pia alikabidhi mifuko 100 ya saruji kwa uongozi wa Kijiji cha Irkaswa Kata ya Kamwanga kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa matatu yanayojengwa kwa nguvu za wananchi huko.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Joseph Ole Sabira alisema msaada wa Dk Kiruswa umekuja wakati muafaka kwa kuwa chama kitakuwa na kumbukumbu za uhakika za wanachama kwa majina na namba za simu.

Alisema hiyo itasaidia kuwa na kura za uhakika za wanachama kwa mgombea Urais, Ubunge na Udiwani wa CCM kutoka ngazi ya chini kabisa.

Katibu wa CCM Longido na Msimamizi wa Uchaguzi ndani ya chama, Ezekiel Mollel amewataka viongozi wote wa chama matawi na kata kutokuwa na mgombea kwani ni kinyume cha taratibu na chama hakitavumilia suala hilo.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Longido

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 4 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...