loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania yaikosha Kamisheni ya Uchumi barani Afrika

WAKATI Tanzania ikitangazwa kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kipato cha kati, Kamisheni ya Uchumi Barani Afrika imesema nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiondoa Kenya, zinaweza kuingia katika kundi la nchi hizo baada ya miaka 20 au 50 ijayo.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Kamisheni hiyo, Carlos Lopes, mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari baada ya Benki ya Dunia kutaja baadhi ya mataifa ya Afrika kuingia katika uchumi wa kipato cha kati.

Kwa mujibu wa Kamisheni hiyo, nchi zitakazoweza kutafsiri maendeleo ya kilimo yaende sambamba na ukuaji wa viwanda, zinaweza kufikia lengo hilo baada ya miaka 20 ijayo yaani mwaka 2040.

Aidha, alisema nchi ambazo zitashindwa kufanya mabadiliko hayo na kuendelea kukumbatia kilimo cha kizamani, zitayafikia malengo hayo baada ya miaka 50 ijayo yaani mwaka 2063.

Kwa mujibu wa Lopes, mataifa ya Afrika Mashariki yaliyoingia katika orodha ya kuwa na uchumi wa kipato cha kati yamesaidiwa na vipaumbele vya kiuchumi vya nchi hizo kuchangia kiwa kiasi kikubwa kuinua uchumi na pato la nchi.

Kati ya nchi za Afrika Mashariki, nchi zilizofanikiwa kuingia katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati ni Kenya ambayo iliingia tangu mwaka 2014 na Tanzania ambayo imeingia mwaka huu kinyume na matarajio yake ambayo ni kufikia hatua hiyo mwaka 2025.

Katibu huyo ndiye mwenye dhamana ya kushajihisha uchumi wa mataifa ya Afrika pamoja na kuratibu mtangamano wa kiuchumi wan chi hizo kwa kutambua na kuhimiza hatua zaidi za kuboresha mtangamano wa kiuchumi.

“Ninafanya kazi kwa karibu na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kuna mawimbi makubwa ya maendeleo katika mataifa mengi ya Afrika. Utulivu wa kiuchumi wa Afrika Mashariki unamaanisha mengi sana,” alisema Lopes.

Alisema kilichoifanya Afrika Mashariki ifanikiwe ni kutokana na kutafsiri maendeleo ya kilimo katika mataifa hayo na kuwa maendeleo ya viwanda yaliyosababishwa na ukuaji wa sekta ya kilimo.

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesisitiza ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi