loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stempu kodi za elektroniki zaongeza mapato TRA

MATUMIZI ya Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) zilizowekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye bidhaa mbalimbali kama vinywaji vikali na sigara, zimechangia ongezeko la asilimia 34 ya mapato yanayokusanywa kwenye bidhaa zenye nembo hiyo.

Aidha, kutokana na ongezeko hilo, TRA imeanza awamu ya pili ya mchakato wa kuweka stempu hizo kwenye vinywaji baridi na kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na tayari viwanda mbalimbali vinavyotengeneza vinywaji baridi, vimeshafungwa mitambo ya kuweka stempu hizo.

Vinywaji baridi hivyo ni pamoja na soda, juisi na maji. Hayo yalisemwa jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo alipotembelea Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba.

Akizungumzia stempu hizo na manufaa yake katika kudhibiti upotevu wa mapato na kudhibiti pia bidhaa bandia, Mbibo alisema mwaka 2018 walianza awamu ya kwanza kuweka stempu hizo za kielektroniki kwenye vinywaji vikali na sigara na matokea yake ni mazuri kwani mapato yameongezeka kwa asilimia 34.

“Uwekaji stempu za kodi za elektroniki kwenye bidhaa ulianza miaka ya nyuma, ila mwaka 2018 tulianza awamu ya kwanza ya uwekaji stempu hizi kwenye vinywaji vikali kutokana na changamoto zake na pia lilikuwa eneo hatarishi na pia kutukusudia kudhibiti vinywaji bandia, matokeo yake ni mazuri sana tumeongeza asilimia 34 ya mapato kwenye bidhaa hizo na kudhibiti vile bandia sasa tumeanza awamu ya pili tutaweka kwenye vinywaji baridi,” alisema.

Alisema baada ya kuweka stempu hizo kwenye vinywaji vikali ilisaidia kuondoa bidhaa za vinywaji feki sokoni na hivyo wenye viwanda kupata masoko na pia kulipa kodi stahiki.

Mbibo alisema hivi sasa wameanza awamu ya pili ya kuweka nembo hizo kwenye vinywaji baridi na sasa viwanda vingi vimeshafungwa mitambo ya kuweka stempu hizo huku mafunzo kwa ajili ya kutumia mtambo huo yanaendelea kutolewa kwa wenye viwanda.

Akizungumzia jinsi TRA ilivyojipanga kuhakikisha inaendelea kutoa huduma zake ili kuifanya nchi izidi kupata kiuchumi, Mbibo alisema wataendelea kubuni njia rafiki za ukusanyaji kodi ili wananchi wafurahie kulipa kodi kwa hiyari.

Akizungumzia iwapo TRA iliathirika na janga la virusi vya corona kwenye ukusanyaji mapato, Mbibo alisema hakuna athari kubwa za kimapato zilizotokea kama ambavyo nchi za nje walizipata.

“Athari hapa kwetu sio kubwa tuliendelea kufanya kazi zetu kama kawaida, ila nchi za nje tuliona nyingi zikifunga mipaka na kuweka amri ya kutotoka, sasa hiyo iliathiri pia viwanda vya nje na kuathiri bidhaa tunazoagiza nje kwa kiasi kidogo hazikuingia kama awali,” alisema Mbibo.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi