loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Michezo ya kubahatisha yaipa Tantrade vifaa kujikinga corona

BODI ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha imekabidhi vifaa mbalimbali kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) vya kuwakinga wananchi wanaoingia kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, James Mbalwe alibainisha kuwa vifaa hivyo vina thamani ya Sh milioni 7.5.

Alivitaja kuwa ni matangi makubwa ya maji 10, kila moja lina thamani ya Sh 500,000, sabuni katoni kumi pamoja na barakoa ambapo alibainisha kuwa jumla ya vifaa vyote ni Sh 7,500,000. Alisema kuwa bodi hiyo inaungana na serikali katika kuhakikisha kuwa maonesho hayo yanaendelea kuwa salama na yenye tija dhidi ya virusi vya corona.

Alisema: “Bodi inatambua nafasi ya Watanzania katika kujenga nchi na ndio maana tumekuja kuwasaidia kuwalinda dhidi ya virusi vya corona na ninawaomba waendelee kuwalinda watoto wasicheze mchezo huu”.

Pia alibainisha kuwa corona imevuruga mapato ya bodi hiyo iliyokuwa ikikusanya kwa kampuni za michezo ya kubahatisha. Alisema kabla ya kuingia virusi vya corona walikuwa wakikusanya Sh bilioni nane kwa mwezi, lakini kwa sasa kwa Juni wamekusanya Sh bilioni 3.7.

Alisema kuwa tangu shughuli zao ziendelee kama kawaida wameanza kuwepo na ongezeko la wateja kucheza tena mchezo huo. Pia alibainisha kuwa bodi hiyo imezindua kampeni ya kuwaepusha watoto kucheza kamari itakayoisha Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Naibu Mtendaji Mkuu wa Tantrade, Ratifah Khamis alisema kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha mazingira salama zaidi kwa wananchi wanaoenda kwenye maonesho hayo.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi