loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Baraza la mawaziri Burundi laapishwa

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa pamoja wameapa kupambana dhidi ya itikadi za mauaji ya kimbari na kutetea na kukuza haki na uhuru wa binadamu nchini Burundi.

Rais huyo amewataka mawaziri hao kufanya kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko ifikapo mwisho wa mwaka huu. Kati ya mawaziri hao 15, wanawake ni wanne na baraza hilo limepunguza ukubwa, ambapo katika utawala uliopita lilikuwa na mawaziri 23. Baadhi ya vyama vya siasa vimepongeza uteuzi huo, huku vingine vikionesha kutokubaliana na uteuzi uliofanywa.

Umoja wa kundi la Twa Ethnic Group Progress (Uniproba), umeshukuru kwa uteuzi wa mwanachama wao mmoja katika baraza hilo la mawaziri. Wakati huohuo, Rais Ndayishimiye ametangaza kampeni maalumu ya kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona na kupunguza bei ya sabuni kwa asilimia 50 kuanzia Juni 30, mwaka huu.

Alitangaza kampeni hiyo baada ya kuapisha baraza hilo la mawaziri, ambapo alisema serikali ppia itapunguza bei ya maji ya kunywa mijini wakati huu ambao kuna maambikizi ya virusi vya corona. Takwimu za nchi hiyo zinaonesha kuwa, watu 170 wameambukizwa virusi vya corona, 115 wamepona na mmoja amefariki.

KIONGOZI wa upinzani, Raila Odinga, amewatahadharisha Wakenya juu ya siasa ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA, Burundi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi