loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watoto zaidi ya 84,000 watibiwa utapiamlo

WATOTO 84,625 waliokuwa na utapiamlo mkali, wametibiwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, licha ya kuwapo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19) nchini Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), limesema licha ya kujikita katika kukabiliana na ugonjwa wa covid-19 kwa wadau wao, lakini linaendelea kutekeleza programu mbalimbali za kutoa huduma za afya na lishe kwa watoto nchini humo.

Taarifa kutoka kwa Mwakilishi wa Unicef nchini Sudan Kusini, Mohamed Ag Ayoya, ilisema wamekuwa wakishughulika na masuala ya magonjwa yanayosababisha vifo kwa watoto kama malaria, maambukizi katika mfumo wa upumuaji na magonjwa ya kuharisha.

“Kwa sababu ya makatazo ya muingiliano wa watu katika kukabili virusi vya corona, tumekuwa tukisafiri maeneo mbalimbali na kusambaza bidhaa nchi nzima, huku baadhi ya programu zikisogezwa mbele au kusitishwa, lakini tuna imani kuwa muingiliano wa watu utaruhusiwa karibuni,” alisema Ayoya.

Katika ripoti iliyotolewa Oktoba 2019, Unicef ilikadiria watoto zaidi ya milioni 1.3 nchini ya umri wa miaka mitano wako hatarini kusumbuliwa na utapiamlo mkali mwaka huu nchini Sudan Kusini na kueleza kuwa, asilimia saba ya watoto wa umri huo wamekuwa wakipata lishe bora.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi