loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Namungo yaipania Simba

TIMU ya Namungo FC imepania kuibuka na ushindi dhidi ya Simba ili kutia doa sherehe za ubingwawa timu hiyo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoutetea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons.

Simba itavaana na Namungo kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, ambako watakabidhiwa taji lao hilo moja kwa moja baada ya kulitwaa mara tatu mfululizo, na wenyeji wao hao wamepania kutia mchanga kitumbua chao.

Akizungumza kutoka Lindi kocha wa kikosi hicho, Hitimana Thiery alisema jana hawawezi kukubali kupoteza mchezo huo, kwani malengo yao ni kupata ushindi kulinda nafasi ya nne wanayoishikilia kwa sasa.

“Ni mchezo mgumu kwa pande zote tunajua Simba wanahitaji ushindi kusherekea ubingwa wao vizuri, lakini sisi hatuitazami Simba tunaangalia ushindi kulinda nafasi yetu ya nne,” alisemaThiery.

Alisema hawawezi kuwaachia Simba kupata ushindi kwenye uwanja huo kwani wana kila sababu ya kuendelea kutunza heshima ya kutokupoteza mechi kwenye dimba lao hilo.

Alisema wanawaheshimu Simba kwani wanakikosi bora ikilinganishwa na timu yao, hivyo wanaingia kwenye mchezo huo wakijua mchezo wa mwisho walipoteza dhidi ya wekundu hao kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na toka hapo hawajapoteza mechi zaidi ya kutoka sare.

Alisema baada ya mchezo huo kikosi hicho kitaanza safari ya kwenda Tanga kwa kuwakabili Sahare All Stars ya Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho (FA) uliopangwa kufanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Wakati huo kikosi cha Simba kimewasili mkoani Lindi kibabe huku kikiwa na morali ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo ili kunogesha sherehe za ubingwa wao sambamba na kujiandaa kwenye mechi dhidi ya Yanga.

Kuelekea kwenye mechi hiyo kocha msaidizi wa kikosi hicho, Seleman Matola amejinasibu kuingia na mbinu mpya itakayowafanya kuchomoza na ushindi kuwapa burudani mashabiki watakaojitokeza kufurahia sherehe hizo.

“Tumejipanga kiushindani na kikubwa tumejipanga kupata ushindi ili kuendelea kuwapa furaha mashabiki wetu kwenye sherehe za ubingwa, ambazo zimepangwa kufanyika baada ya kumalizika kwa mechi,” alisema Matola.

Simba ilitangazwa bingwa baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons na kufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Simba sasa ina pointi 80, huku Azam iliyorudi katika nafasi ya pili baada ya juzi usiku kuifunga Singida 7-0, ina pointi 62 huku Yanga ikirejea katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 61.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi