loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara wajiandaa soko jipya Kisutu

WAFANYABIASHARA wa soko la zamani la Kisutu jijini Dar e s salaam wamefurahishwa na ujenzi wa soko jipya la kimataifa unaoendelea katika eneo hilo ambao unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es saaalm, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, waliotembelea kujionea maendeleo ya soko hilo, walisema ujenzi huo ni fahari kwao kwa kuwa utawaweka katika mazuri ya kufanya biashara.

Mmoja wa wafanyabiashara hao sokoni hapo aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Hassan alisema kimsingi ujenzi huo unaenda kutatua changamoto zote ambazo walikuwa wakikumbana nazo mahali hapo.

Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Amina Shaban aliipongeza Serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwajengea soko hilo.

“Naipongeza Serikali kwa ujenzi unaoendelea wa soko hili, hii ni ishara ya dhati kuwa Serikali yetu imeonesha kutujali sisi wafanyabiashara wadogo na ningependa kuishauri serikali kuhakikisha haki na usawa unatendeka pindi watakapoanza kugawa maeneo ya biashara baada ya kukamilika kwa soko hilo, “ amesema Amina.

Ujenzi wa soko hilo la kisasa umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwezi wa Nane mwaka huu na kuchukua wafanyabiashara 1,500 huku kukiwa na huduma nyingine za kijamii kama benki, machinjio ya kuku, ofisi mbalimbali pamoja na ukumbi wa mikutano.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwanahija Said, Udom

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi