loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chai Bora waishukuru serikali kusaidia viwanda

KAMPUNI ya Chai Bora imesema licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini, Serikali imeendelea kuwasaidia wazalishaji wa viwanda vya ndani kutafuta masoko ndani na nje ya nchi huku ikichukua tahadhari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam, Meneja Masoko wa Chai Bora, Awatif Bushiri alisema serikali imefanya jitihada kubwa za kusaidia viwanda vya ndani kuhakikisha vinazalisha bidhaa bora.

“Kama inavyojidhihirisha kwenye kauli mbiu ya mwaka huu isemayo Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu, serikali imeweka mazingira mazuri na kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kipato cha kati kupitia viwanda,” alisema Bushiri.

Alisema wao kama watengenezaji na wafungashaji maarufu wa chai nchini, wanalenga kuuza bidhaa zao katika masoko ya nje katika nchi za Kenya, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu, Rwanda na Ghana na kwamba maonesho hayo ni moja ya njia wanazotumia katika kukuza usambazaji wa bidhaa zao.

Alieleza kuwa asilimia 90 ya bidhaa wanazozalisha ni kutoka ndani ya nchi na kwamba malighafi hizo hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile viungo na lishe.

Kwa mujibu wa Bushiri, Sekta ya Kilimo imesaidia nchi kuingia kwenye uchumi wa kati kwa sababu takribani asilimia 75 ya nguvu kazi huishi katika maeneo ya vijijini na wengi wao wanajishughulisha na shughuli za kilimo ambacho huchangia asilimia 50 ya Pato la Taifa.

“Chai Bora inajivunia kuwa na bidhaa zinazotumika na Watanzania wengi na inavijunia nafasi za ajira zinazotengenezwa kuanzia viwandani mpaka mashambani malighafi huzalishwa,” alisema Bushiri na kuongeza.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi