loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara yataka ubunifu kukuza uchumi

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo, amewataka Watanzania kuwa wabunifu katika nyanja ya sayansi na teknolojia ili kukuza uchumi wa viwanda, ajira na biashara endelevu.

Alitoa mwito huo juzi wakati wa majadiliano kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kwenye viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.

Majadiliano hayo yalishirikisha wadau mbalimbali, ikiwamo Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Shirika la Viwanda Vidogo (Sido), Mamlaka ya Vyuo vya Ufundi Stadi (Veta), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na wengineo.

Alisema kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati, hivyo inahitaji maendeleo katika sekta ya viwanda na uzalishaji ili kukuza zaidi uchumi wa nchi.

Akwilapo alisema Tanzania ina wabunifu wengi wa teknolojia, lakini wanashindwa kukuza kipato chao kutokana na kuzalisha bidhaa ambazo zinakosa masoko.

“Kuna wabunifu wengi sana katika masuala ya ufundi na teknolojia, lakini wengi wao wanakosa njia bora ya kuboresha kazi zao na kujikuta wanazalisha bidhaa ambazo zinakosa soko katika ushindani. Kinachotakiwa hapa ni kuboresha bidhaa zao na kukidhi haja ya mlaji katika masoko ambako kuna ushindani wa hali ya juu,” alisema.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, inatilia mkazo maendeleo katika sekta ya viwanda ili kukuza uchumi wa wananchi.

Katika majadiliano hayo, mada kuu tatu zilijadiliwa zenye lengo la kuendeleza na kukuza uchumi wa viwanda, kuongeza ajira na biashara.

Majadiliano hayo yalikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu unaotokana na ushiriki katika ubunifu na ujasiriamali, mchango wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu (STU) katika kuchochea maendeleo ya sekta ya viwanda na mambo yanayotakiwa kufanyika ili kuwezesha sekta binafsi kuongeza ushiriki katika kuchangia maendeleo ya utafiti na ubunifu.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu, alisema majadiliano hayo yameleta tija kwa wadau na kuwa kichocheo cha maendeleo katika sekta hiyo na ubunifu.

Alisema katika kuhakikisha sekta ya teknolojia na ubunifu inaendelea, Costech imeanzisha mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu (Makisatu), ambayo hufanyika kila mwaka ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Alisema mashindano hayo yanashirikisha wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka vyuo kikuu na Costech imekuwa ikitoa fedha kwa washindi ambao wanahitaji kuboresha kazi zao za ubunifu.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi