loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ahimiza utafiti zaidi zao la ngano

UTAFITI zaidi wa zao la ngano unahitajika hivi sasa kutokana na kukua kwa mahitaji yake.

Imeelezwa kuwa wakati taifa linazalisha kati ya tani 64 hadi laki moja, mahitaji yake ni tani milioni moja.

Hayo yalibainishwa na Mtafiti wa zao la ngano katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari), Kituo cha Uyole mkoani Mbeya, Dk Rose Mongi alipokuwa akizungumza na HabariLeo.

Dk Mongi alisema utafiti huo ni muhimu kwa kuwa watu wengi wanatumia ngano katika matumizi mbalimbali kama vitafunwa ikiwemo mikate, chapati na vinginevyo hivyo kuilazimu nchi kuagiza ngano zaidi nje ya nchi kukidhi mahitaji.

“Uzalishaji ni kati ya tani 64 hadi laki moja. Mahitaji ni tani milioni moja zaidi ya tani laki nane nchi inaagiza kutoka nje kufidia pengo hilo,” alisema Dk Mongi.

Alisema kituo hicho kinatafiti mbegu bora za ngano zinazoendana na mazingira yaliyopo ili kuweza kumaliza tatizo hilo la kuagiza nje ya nchi.

Alisema endapo nchi itaweza kuzalisha hekta laki tatu itakuwa imekidhi mahitaji yanayohitajika.

Alitaja mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inayozalisha ngano kuwa ni Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Songwe na wilaya ya Mbinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Uyole, Dk Tulole Bucheyeki alisema wanazalisha mbegu bora za zao hilo pamoja na kutoa utaalamu ili wakulima waondokane na kilimo cha kujikimu walime kilimo cha kibiashara.

Mkurugenzi Mkuu wa Tari, Dk Geofrey Mkamilo alisema taasisi hiyo inahakikisha teknolojia mbalimbali ambazo zimegunduliwa zinawafikia wakulima kwa kuwa itakuwa haina maana zisipokuwa na mchango wowote kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

Mtafiti wa zao la ngano Kituo cha Utafiti Selian mkoani Arusha, Nafeti Mheni alisema hivi sasa nchi huagiza ngano kutoka nje kwa gharama ya takribani dola milioni 225 kwa mwaka.

Alisema Kituo cha Uyole kwa kushirikiana na Selian, vimetafiti mbegu mpya za ngano zenye sifa na ubora ambazo ni Merina, Shangwe na Ngoli.

Alisema uzalishaji huo mdogo haupo kwa Tanzania pekee bali ni changamoto ya nchi za Afrika kwa ujumla kwa sababu kwa ujumla nchi za Afrika zinazalisha tani milioni 25.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi