loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii WCB kufanya yao Tanga

MSANII nguli wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametangaza kufanyika kwa shoo yake ya kwanza ya wasanii wa lebo ya WCB, ikiwa ni miezi kadhaa tangu janga la virusi vya corona liibuke na kusababisha mambo mengi kusimama.

Shoo hiyo imepangwa kufanyika mkoani Tanga mwezi ujao, ingawa hajaweka wazi tarehe na siku wanayotarajia kuwaburudisha wapenzi na wafuatiliaji wa muziki wanaofanya kazi chini ya lebo ya WCB, ambayo Platnumz ndiye rais wake.

Akizungumza Dar es Salaam, Diamond alisema ana mpango wa kushiriki kwenye shoo hiyo kwa kuwa promota, Ali Babu, ameweka kiasi kidogo cha fedha, lakini kama atakuwa tayari kuongeza atakuwa miongoni mwa wasanii watakaopanda jukwaani kutoa burudani.

“Tumekaa muda mrefu bila kufanya shoo, lakini kama WCB tunatarajia kuanza kufanya hivyo mkoani Tanga na wasanii wa lebo yangu watakuwa wanapanda jukwaani, lakini mwenyewe huenda nisishiriki kama promota hataongeza dau,” alisema Platnumz.

Alisema shoo hiyo itakuwa na ubora wa kipekee na kuwaomba mashabiki wa mkoa huo kuanza kufanya maandalizi katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kwa ajili ya kuhudhuria kwenye tamasha hilo baada ya shughuli za muziki kusimama kwa kipindi cha miezi minne sasa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 18 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...