loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Billnas- Nipo siriasi nitamuoa Nandy

MSANII wa muziki wa kizazi kipya , Wiliam Lyimo ’Billnass’, ameeleza changamoto za kuyumba kiuchumi ni miongoni mwa sababu zinazochelewesha kufunga ndoa yake na muimbaji, Faustina Mfi nanga ‘Nandy’, licha ya kuvalishana pete miezi miwili na nusu iliyopita.

Rapa huyo amedai kwa sasa anashughulikia changamoto hiyo kwa kuweka mambo sawa ili akimuoa mrembo huyo aishi maisha kama malkia na sio kupata shida.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Billnas alisema kulipuka kwa ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona ndiko kulikosababisha avuruge mipango yote waliyokubaliana kufunga ndoa ambayo anadai ingekuwa mfano wa kuigwa kwa mastaa wengine Tanzania.

“Mpango wa kufunga ndoa na Nandy umebaki vilevile kwa kuwa ni binti wa kwanza kumvalisha pete katika historia ya maisha yangu na kwenye hili siwezi kuleta mzaha kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiri ni kiki,” alisema Billinas.

Alisema anaamini kwa uwezo wa Mungu atafunga ndoa na mrembo huyo ambaye amejizolea umaarufu kwenye tasnia ya sanaa kwa kuimba nyimbo kiasi cha kuwa miongoni mwa wasanii ambao nyimbo zao zinapendwa na mashabiki wengi.

Alisema pamoja na mambo kwenda ovyo, amejipanga mwishoni mwa mwaka huu watafunga ndoa ili waanze kuishi pamoja kupanga mipango ya kuwa na familia kama mama na baba.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...