loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa: Tutaimarisha usafiri wa majini

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema malengo ya serikali ni kuimarisha usafi ri kwenye maziwa yote na bahari, ili kuwawezesha Watanzania wafanye biashara na mataifa ya nje.

Alisema hayo alipozungumza na wananchi katika viwanja vya Klabu ya Bandari mjini Mtwara jana jioni. Majaliwa alisema kabla ya kukagua ujenzi wa Gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara, juzi alitembelea miradi ya ujenzi wa bandari za Karema mkoa wa Katavi, na Kabwe na Kasanga mkoani Rukwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.

“Malengo yetu ni kuruhusu mataifa ya nje yafanye biashara na Tanzania na kuruhusu Watanzania wasafiri kwenda hukohuko kuona na kujifunza ili warudi hapa na taaluma mpya. Utaratibu huo pia utawezesha kutengeneza mzunguko mzuri wa kifedha kwa wananchi,”.

“Nimetoka Ziwa Tanganyika ambako tunapakana na Burundi, Rwanda, Zambia na Congo na serikali kwenye mkakati huu tumeingiza fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa bandari zetu. Tumeimarisha Bandari ya Kigoma pale Kibirizi, kazi imekamilika na sasa tunajenga eneo la kuweka makontena” alisema Waziri Mkuu.

Alisema katika Ziwa Victoria kuna meli iliyokuwa inakarabatiwa, imeanza majaribio ya kwenda Kagera na nyingine inaendelea kujengwa, ili kuruhusu wafanyabiashara wa Kanda ya Ziwa wafanye biashara zao kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka vijana wanaopata ajira kwenye miradi mikubwa inayogharimiwa na serikali, watumie fursa hiyo kupata utaalamu, utakaowawezesha kuajiriwa maeneo mengine hata baada ya miradi ya sasa kukamilika.

Alisema hayo wakati akizungumza na vijana wa Kitanzania wanaofanya kazi kwenye mradi wa gati jipya katika bandari ya Mtwara jana mchana. Awali, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Juma Kijavara alimweleza Waziri Mkuu kuwa kazi ya ujenzi wa gati namba 2 katika bandari ya Mtwara, inafanywa na kampuni ya China Railway Construction Enginereering Group Limited (CRMBEG).

Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi Mei 27, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu. Mradi huo umefikia asilimia 75 ya utekelezaji wake na Sh.bilioni 74.84 zimeshalipwa kwa mkandarasi, sawa na asilimia 48.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Mtwara

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi