loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jafo awatwisha mzigo ma-RC

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa miezi miwili kwa wakuu wa mikoa wote nchini, kuhakikisha fedha ambazo hazijaingia kwenye mfumo wa serikali, zinaingizwa zote.

Pia amewataka wateule wa rais, kuhakikisha Sh bilioni 170 zilizotumwa kwenye akaunti zao hivi karibuni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika kuondoa msongamano madarasani, zinasimamiwa vizuri na miundombinu hiyo inakamilika ndani ya miezi mitatu ijayo.

Alitoa agizo hayo jijini hapa wakati wa kuwakabidhi nyenzo za kufanyia kazi wateule wapya, ambao ni wakuu wa mikoa wawili, katibu tawala wa mkoa mmoja, wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi wa halmashauri nane.

Alisema wakuu wa mikoa hao, wanatakiwa kuhakikisha fedha zote za serikali, ambazo ziko nje ya mifumo ya ukusanyaji mapato, ni lazima ziingizwe ndani ya miezi miwili.

“Kuna fedha za serikali za mwaka wa fedha uliopita, ambazo mpaka sasa ziko nje ya mifumo, iwe kwa bahati mbaya, au kwa wizi au madeni, ni lazima ziingizwe kwenye mifumo ya mapato ya serikali; na kazi hii wakuu wa mikoa wote muwe mmeikamlisha ndani ya miezi miwili,”alisema.

Hata hivyo, Jafo alisema ajenda ya ukusanyaji mapato ni ya kudumu. Aliwataka wateule hao, kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kusimamia matumizi yaliyo sahihi na pia fedha za miradi ya maendeleo zinapelekwa.

“Kwenye ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zetu changamoto kubwa ilikuwa ni upotevu wa mapato na ndio maana Tamisemi tuliamua kununua mashine za kielekroniki 7,227 na kuzigawa katika halmashauri zote, lengo likiwa ni kutimiza ajenda ya kukusanya mapato ipasavyo na kudhibiti mianya ya upotevu.

Alisema “Msiende kukaa maofisini kama ilivyo kwa fundi cherehani, nendeni site (maeneo ya miradi) mfuatilie kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, serikali imetoa na inatoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali hivyo mkafanye kazi kwa nguvu zenu zote’’.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi