loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa kukabidhi Simba taji

KOCHA wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema anatamani kupata pointi tatu ili kujiweka katika nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye atakaye kuwa mgeni rasmi, akitarajiwa kuwakabidhi Simba taji baada ya mchezo huo.

Namungo FC, leo itakuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa mjini hapa. Akizungumzia mchezo huo, Hitimana alisema Simba haina chakapoteza ila wao wanahitaji kupata ushindi kujiweka katika nafasi za juu.

Katika mchezo huo, kiingilio cha VIP ni Sh 10,000 na mzunguko ni 5,000, na viingilio vimekuwa vikitozwa kwa mechi zinazohusisha Simba na Yanga na wenyeji hao ili kudhibiti idadi ya watu, lakini kwa michezo mingine hakuna kiingilio.

Uwanja wa Majaliwa bado upo kwenye matengenezo hasa jukwaa pamoja na vyumba vya wachezaji na vya waamuzi na hadi sasa umekamilika kwa asilimia 50, lakini eneo la kuchezea kwa maana ya uwanja ni nzuri.

Simba inatarajiwa kuwasili leo kwani baada ya mechi ya Ndanda waliendelea kubaki Mtwara na wakimaliza mechi wataondoka leo baada ya sherehe za ubingwa.

Mabingwa hao walithibitisha ubingwa huo Jumatano iliyopita walipotoka suluhu na Tanzania Prisons na kufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi hiyo.

Kwa sasa Simba na pointi 80. Wakati huo huo, Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema mchezo dhidi ya Kagera Sugar ni muhimu kwao kupambana na kupata matokeo mazuri ili waweze kurudi katika nafasi ya pili.

Yanga iliyokuwa inashika nafasi ya pili ilirudishwa kwenye nafasi ya tatu baada ya kutoka suluhu mchezo uliopita dhidi ya Biashara United, huku Azam ikipanda kufuatia kushinda mchezo wake, dhidi ya Singida United.

Kwa mujibu wa ratiba mechi zingine leo ni Tanzania Prisons itacheza na coastal Union, Azama dhidi ya Mwadui, Biashara dhidi ya Ruvu Shooting, Mbao na Mtibwa, Ndanda na JKT Ruvu na KMC dhidi ya Singida United.

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo, Ruangwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...