loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yapamba kila kona Ruangwa

MITAA ya mji wa Ruangwa imepambwa kwa bendera za rangi nyekundu na nyeupe zikiashiria kuwa kuna jambo la kihistoria linakwenda kutokea katika mji huo.

Simba leo inacheza na Namungo katika mchezo wa kukamilisha ratiba kwa Wekundu hao wa Msimbazi katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo.

Kwenye Uwanja wa Majaliwa, Simba leo itacheza na wenyeji Namungo FC, na baada ya mchezo huo watakabidhiwa taji lao la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2019- 2020.

Uwanja wa Majaliwa kwa upande wa sehemu ya kuchezea ni mzuri ila kwa upande wa vyumba vya kuvalia wachezaji, waamuzi na majukwaa kazi inaendelea haijakamilika na wanafanya kazi usiku kucha kwa kutumia taa ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza kwa mchezo huo leo jioni.

Kazi ya kupaka rangi ilianza juzi na pamoja na ile ya kuweka talazo kwenye vyumba vya wachezaji vya kubadilishia nguo na vile vya waamuzi ili wapate sehemu ya kukagulia timu.

Lakini wakati maandalizi hayo yakiendelea, nyumba za kulala tangu juzi zilikuwa zimejaa kutoka na kujaa mashabiki wa Simba pamoja na kuendelea kwa mashindano ya Ligi Daraja la Pili hatua ya Sita Bora kuendelea hapa.

Kuna timu sita, viongozi wa timu na wasimamizi wa mashindano, ambapo vyumba vimejaa na kuifanya African Sports kukosa mahali pa kulala, na imewabidi kufikia katika nyumba isiyokamilika na kuwekewa magodori chini kwa ajili ya kulalia.

Hali hiyo imeikuta pia Simba, ambayo baada ya kucheza na Ndanda FC ikabidi iendelee kukaa huko huko Mtwara na leo ndio itakwenda Luangwa na kufikia moja kwa moja uwanjani na baada ya mchezo huo watakabidhiwa kombe lao na kuondoka leo kurudi Dar es Salaam.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...