loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mradi wa maji wa milioni 612/- wazinduliwa Milonji

MWENYEKITI wa Chama Kikuu cha Ushirika cha wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI), Hassan Mpako amewataka wanachama wa chama hicho kutumia vyema nafasi ya kukopa pembejeo ili kuimarisha zao la korosho.

Akihutubia wakulima katika mnada uliofanyika kijiji cha Ikungi wilayani Nachingwea alisema kwamba RUNALI imefanya kazi ya ziada ya kuomba mkopo wa pembejeo na kutaka wanachama wake kukopa na kuwa na uaminifu wa kurejesha fedha.

“Tunajua msimu uliopita soko la korosho lilikuwa na matatizo makubwa, hivyo sisi tukahangaika kupata mkopo wa pembejeo,” alisema Mpako na kuongeza kuwa kama fedha hizo zisipolipwa chama hicho kitapoteza uaminifu na kukwama kwa maendeleo ya wakulima.

Alisema wamebaini kwamba wanachama wake wanalanguliwa pembejeo aina ya salfa na hivyo wao kama chama kikuu wametafuta utaratibu ambao kama ukitekelezwa kama ulivyopangwa chama hicho kitakuwa kimejenga uwezo wa kusaidia wakulima wakati wote. Alisema chama hicho kinatoa pembejeo hiyo kwa Sh 32,000 ambazo zinaweza kulipwa taslimu au nusu au kwa mkopo.

“Najua kuna watu wamelanguliwa, wanauziwa kwa mkopo salfa ya Sh 35,000 kwa malipo ya Sh 40,000. Mnaweza kufanya mpango na Amcos zenu kwa kujirodhesha kupata mkopo huo au pembejeo hizo lakini ukikopa usikimbie,” alisema Mpako.

Alisema pamoja na pembejeo hiyo kuletwa pia katika kukopeshana bodi zinatakiwa kutazama kama anayekopeshwa analipa au ana historia ya kutolipa mikopo.

“Kama una historia ya kutolipa mikopo hutapewa. Lakini niseme ukishapewa wakati wa mauzo ya korosho zako usibadili jina ili kukwepa kulipa au kuuza katika chama kingine,” alisema Mpako, na kuongeza kuwa kitendo hicho kitasababisha dhamana ya Runali kuonekana kuwa na walakini na hivyo kutoaminika tena.

Alisema ni kazi ya chama hicho kuhakikisha kwamba wanachama wake wanapata nafuu katika shughuli zao na kutokana na serikali kukamilisha ushawishi kwa benki kuhusu mikopo kwa wakulima ni vyema wakulima nao wakarejesha uaminifu na kuendeleza kilimo chao.

“Tutumie vyema dawa hiyo; pembejeo hii sio sadaka ni mkopo ni lazima kuulipa, tusipolipa mikopo, Runali itaingia katika matatizo na wakulima pia watakuwa na matatizo, haya ni mabilioni ya fedha,” alisema Mpako.

Aidha aliwataka wakulima pia kuepuka migororo ya malipo kwa bidhaa wanazouza kwa kuwa na jina halisi katika cheti cha kuingiza bidhaa ghalani na akaunti yake ya benki.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Nachingwea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi