loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kiroho kwatu

SIMBA imekabidhiwa rasmi Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kutoka suluhu dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Simba pamoja na wiki iliyopita kujihakikishia ubingwa baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya na kufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, ilikabidhiwa kombe hilo jana.

Kwa sare hiyo, Simba sasa ina pointi 81 ikiendelea kutamba huku wenyeji wao Namungo wakifikisha pointi 60 na kuendelea kubaki katika nafasi yao ya nne katika mbio hizo za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2019/2020.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ndiye aliyemkabidhi nahodha wa Simba, John Bocco kombe hilo la 21 kwa timu hiyo, ambalo wamelitwaa kwa mara ya tatu mfululizo na kuwa lao kabisa.

Awali, ilielezwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ndiye angekabidhi kombe hilo kwa vijana hao wa Simba. Mbali na Dk Kigwangalla pia alikuwepo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia pamoja na wageni wengine waalikwa.

Wachezaji wa Simba walivalishwa medali za dhahabu mmoja baada ya mwingine kabla ya nahodha wao, Bocco kukabidhiwa kombe hilo. Katika mchezo huo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu huku kila upande ukikosa mabao na kufanya kwenda mapuziko wakiwa sare ya bila kufungana, matokeo ambayo yalikwenda hadi mwisho wa mchezo huo.

Namungo nusura wapate bao katika dakika ya 45 wakati Kelvin John aliposhindwa kufunga akiwa ndani ya meta 18 baada ya kupata pasi ya Abeid. Kikosi cha Namungo kilikuwa; Nourdine Balora, Miza Christom, Edward Manyama, Stephen Duah, Carlos Protas, Hamisi Khalifa, Hashim Manyanya/Jamal Issa (dk73), Steve Nzigamasabo, Bigirimana Blaise/John Kelvin (dk31), Lucas Kikoti na Abeid Athumani.

Simba SC; Beno Kakolanya, Haruna Shamte/Hassan Dilunga (dk 63), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Tairone Santos/Gardiel Michael (dk 52), Said Hamisi, Miraji Athumani ‘Madenge’, Muzamil Yassin, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu/Cyprian Kipenye (dk 71) na Francis Kahata/ Deo Kanda (dk 63).

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo, Ruangwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 21 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 21 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 21 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...