loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Morrison ifungia tena Yanga

MABINGWA wa kihostoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana walirejea kwa muda katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 64 na kuishusha Azam FC yenye pointi 62 katika nafasi hiyo, ambao jana usiku ilikuwa ikpepetana na Mwadui ikitafuta ushindi ili kurejea katika nafasi yao ya awali.

`Mtukutuku’ Bernard Morrison, ambaye aliifuata Yanga mapema jana kwa ndege, ndiye alikuwa shujaa wa timu hiyo baada ya kufunga bao katika kipindi cha pili na kurudisha shangwe Jangwani.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alifunga bao hilo baada ya ushirikiano na wachezaji wenzake na kuujaza mpira huo wavuni katika dakika ya 78.

Yanga na Azam zimekuwa zikifukuzana katika mbio za kuwania nafasi ya pili baada ya ile ya kwanza kushikwa na Simba iliyotetea ubingwa wake na kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika msimu ujao.

Matokeo mengine jana; KMC iliibuka na pointi zote tatu baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 2-0, huku Mbao ikishinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Biashara ikitoka suluhu na Ruvu Shooting na Simba ikitoka sare na Namungo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 22 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 22 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 22 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...