loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yajipanga kununua ndege ya mizigo

SERIKALI ipo katika hatua za awali za kununua ndege yake ya mizigo, kwa ajili ya usafirishaji wa mazao, matunda na maua kwenda moja kwa moja katika soko la Ulaya, bila kupitia nchi za kiafrika.

Pia tayari mazungumzo ya ujenzi wa meli katika Bahari ya Hindi umeanza ili kumpunguzia mfanyabiashara gharama za usafirishaji wa mizigo kwenda soko la Ulaya.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashansta Nditiye alisema hayo katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) wakati akikagua shughuli za usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi.

“Mwezi Aprili nilifika hapa kuzindua ndege ya mizigo ya Ethiopia Airlines kupeleka mizigo nje ya nchi, kwa kipindi cha miezi mitatu tumefanikiwa kusafirisha zaidi ya tani 590 za mizigo kwenda nje ya nchi ikiwamo Ulaya,”alisema.

Alitaka wafanyabishara wa ndani kutumia viwanja vya ndege vya ndani ya nchi kwani wataweza kuokoa zaidi ya Dola za Marekani 4,000 katika kusafirisha mizigo isiyozidi tani 10 kwa safari moja.

Alisena serikali imeondoa changamoto katika bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga na kutoa mfano bandari ya Tanga ambayo imetanuliwa na sasa meli inaweza kufika eneo la gati badala ya kutia nanga umbali wa kilometa mbili kutoka mzigo ulipo.

Alipongeza wanachama wa Chama cha Wakulima wa Mbogamboga na Maua Tanzania (Taha) ambao wamehamasisha wafanyabishara na wakulima ambao sasa wanasafirisha mazao yao moja kwa moja katika uwanja wa KIA badala ya kupitia nchi jirani.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Kadco, Mary Kimambo alisema wamefanikiwa kutanua eneo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mazao yanayoharibika kwa haraka ikiwamo matunda, mbogamboga na maua.

Alisema ndege ya Ethiopia Airlines imekuwa ikifanya safari mara tatu kwa wiki ambapo wamefanikiwa kuongeza usafirishaji wa mizigo hususan mazao na matunda ikilinganishwa na abiria.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Hai

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi