loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kigaigai aishauri Veta kuongeza ubunifu

KATIBU wa Bunge, Stephen Kigaigai ameitaka Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), iongeze ubunifu na iwaimarishe zaidi vijana wanaopata mafunzo katika vyuo vyao hasa kwenye masuala ya ufundi na uendelezaji wa ubunifu wao.

Kigaigai alisema hayo Dar es Salaam jana alipotembelea banda la Veta, kwenye Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba, ambapo alisema mamlaka hiyo imekuwa ikitoa mafunzo bora yanayoendana na kaulimbiu ya sera ya uchumi wa viwanda.

Aidha Kigaigai aliishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuweka msisitizo kwa mamlaka hiyo kuwa na utaratibu wa kuwafuatilia vijana wanaohitimu mafunzo yao na kujua kama wanaendeleza vipaji vyao vya ufundi.

"Veta na Wizara ya Elimu wanatakiwa kushirikiana kuwafuatilia vijana hawa wanapomaliza masomo yao hasa kuangalia wanapokwenda na wanafanya nini," alisema Kagaigai.

Hata hivyo, Meneja Mawasiliano kutoka Idara ya Uhusiano wa Veta, Peter Sitta alisema walifanya tathmini ya mwaka 2018 kufahamu wahitimu wao wako wapi na wanafanya nini.

Alisema jumla ya wahitimu 3,213 walifanyiwa tathmini ambapo ilibainika kuwa wahitimu 1,015 sawa na asilimia 32 ya wahitimu hao wameajiriwa huku wengine 311 sawa na asilimia 10 wameajiriwa na kuajiri wengine na wahitimu 895 wamejiajiri sawa na asilimia 28.

Sitta alifafanua kuwa wahitimu 88 sawa na asilimia tatu wanafanya kazi kwenye karakana na ofisi za familia bila malipo huku wale wanaojitolea wakiwa ni 66 sawa na asilimia mbili na wale wanaofanya mazoezi ya vitendo ni 26 sawa na asilimia moja.

Aidha wale waliomaliza masomo na kuendelea na masomo mengine ngazi ya juu zaidi ni 150 sawa na asilimia tano na wale wanaotafuta kazi ni vijana 357 sawa na asilimia 11 ila pia vijana 269 sawa na asilimia tisa hawana ajira wala hawatafuti kazi.

"Tulifanya tathmini mwaka 2018 kujua wako wapi wahitimu wetu 3,213, tulibaini kwamba wapo waliojiajiri na kuajiri wengine, lakini pia wapo walioajiriwa na wengine wanafanya kazi kwenye karakana za familia, lakini pia wapo wasiotafuta ajira," alisema Sitta.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi