loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NFRA kutumia bil 30/- kununua mahindi

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi msimu wa ununuzi wa mahindi kwa kuyanunua kwa Sh 550 kwa kilo.

Aidha serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa mahindi takribani tani 500,000.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Vwawa, mkoani Songwe jana, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, alisema msimu huo umeanza tangu Julai 6 na kwamba kila mtu anaturuhusiwa kuuza mahindi kwa wakala huo.

“Napenda kuwajulisha kuwa, mtu yeyote anaruhusiwa kuuza mahindi NFRA bila upendeleo wowote, ilimradi mahindi hayo yawe na ubora unaotakiwa,” alisema. Akifafanua zaidi Sh bilioni 30 zilizotengwa Waziri Hasunga alisema kuwa zitatolewa na serikali kuu.

“NRFA ina majukumu mawili ambayo ni kununua chakula kutoka kwa wakulima na kuhifadhi kwa ajili ya akiba kwa Taifa ,pamoja na kuuza kwa nchi zinazopata matatizo ya upungufu wa chakula na katika bajeti ya fedha ya mwaka uliopita ilitengewa shilingi bilioni 15 na mwaka huu pia tumetenga shilingi bilioni 15.

“ Lakini tunazo fedha tuliuza mahindi yetu kule Zimbabwe na tayari walishatoa, hivyo kwa ujumla wake serikali tutatoa kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa mahindi hayo” alifafanua Hasunga.

Aidha, Waziri Hasunga aliitaka NFRA kwenda kukopa fedha katika taasisi za kifedha kwa ajili ya kununua mahindi zaidi kutoka kwa wakulima.

Hasunga alisema kutokana na mkoa wa Songwe kushika nafasi ya tatu kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini, katika msimu wa 2018/19, serikali imeanzisha Kanda ya NFRA katika mkoa huo. Kanda ya NFRA Songwe ilianzishwa rasmi Julai Mosi, mwaka huu na inahudumia mikoa ya Songwe na Mbeya.

“Kuanzishwa kwa kanda hii kumetokana na hali ya uzalishaji mkubwa wa chakula katika mikoa ya Songwe na Mbeya, pamoja na kujengwa kwa maghala na vihenge vya kisasa ambavyo vitaongeza uwezo wa uhifadhi kutoka tani 17,000 za awali na kufikia tani 37,000,” alisema.

Hasunga alisema NFRA katika kanda hiyo, msimu huu inaanza na ununuzi wa mahindi tani 10,000. Wakati huohuo, waziri huyo alizungumzia Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kila mwaka kuanzia Agosti 1-8.

“Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa, maonesho ya Nane Nane kwa mwaka 2020 yatafanyika kwenye kanda nne, yakiwa ni ya 28 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993,” alisema. Alizitaja kanda hizo kuwa ni: Mashariki (Morogoro), Kaskazini (Arusha), Magharibi (Tabora), Kusini

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Songwe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi