loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sitaongeza hata dakika moja madarakani -Shein

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais Dk Ali Mohamed Shein (pichani) amesema kuwa hataongeza dakika moja madarakani. Amesisitiza kuwa hana shaka Dk Hussein Mwinyi, kwani ataitumikia Zanzibar kwa umahiri mkubwa sana.

Alisema hayo wakati wa kuwaaga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini hapa jana. Alisema kwa kuwa yeye ni kiongozi aliye- chaguliwa kwa msingi wa katiba, hivyo atahakikisha haongezi hata dakika moja kuwa madarakani.

“Mwezi wa kumi mwaka huu Mungu akip- enda tunafanya uchaguzi mkuu wa rais, kwa hivyo hapana shaka chama chetu kitaibuka mshindi. Kwa uwezo wake na uzoefu wake na sina shaka Dk Hussein atakivusha chama chetu huko Zanzibar kwa ushindi mkubwa.

“Na kwa sababu mimi ni kiongozi wa kitaifa, sitapata nafasi ya dakika moja kuongeza muda niwe Rais wa Zanzibar. Katiba hainiruhusu, chama changu hakiniruhusu kwa sababu muda wa kuondoa umefika. Chama changu hakiniruhusu, kimesham- chagua mwingine, kwa hivyo nitalazimika kukikabidhi kijiti cha rais wa Zanzibar kwa mwana-CCM mwenzangu Dk Hussein Mwinyi,” alisema.

Dk Shein alisisitiza kuwa Dk Mwinyi ni chaguo sahihi, kwani ana uhakika kuwa ana uwezo kuwatumikia wananchi wa Zanzibar “Jana nimepata faraja sana, baada ya kukamilisha mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais Zanzi- bar ambaye anakuja kuni- pokea na kunipumzisha mzigo huu mzito.

Nilipata furaha kubwa baada ya Dk Hussein Mwinyi kuchagu- liwa kama mgombea wa Zanzibar. Nilipata fursa kwa kuwa ni mtu ninayem- fahamu. Kama alivyosema nilipokuwa Makamu wa Rais alikuwa waziri katika ofisi yangu anayeshughulikia Muungano.

Alifanya kazi vizuri sana, alifanya kwa umahiri mkubwa. “Sina shaka nafasi hii kwa Zanzibar ataitumikia kwa umahiri mkubwa sana, Dk Mwinyi maana njia yenyewe ameishaanza kuijua, mambo ya Muun- gano ni moja ya mambo katika Jamhuri ya Muungano.

Anayajua kayafanyia kazi na sasa ataogelea kwenye bahari hii na sote tunajua kwamba mwamba ndio msingi wa bahari wa mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano,” alisema. Aidha, Dk Shein aliwapongeza viongozi waliomsaidia kuanza safari ya uongozi ndani ya chama na serikali.

“Namshukuru Rais mstaafu Dk Salmin Amour aliyeniteua kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar baada ya uchaguzi kwenye jimbo la Mkanyageni kufanyiwa mchezo wa rafu na chama cha upinzani na kwa kauli ya kwamba nimeshindwa uchaguzi ule, yeye aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Afya.

“Pia naomba nimshuku- ru kwa dhati Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Dk Amani Abeid Karume aliyeniteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora mwaka 2000 hadi nilipoteuliwa baadaye na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa kuchukua nafasi ya Makamu wa Rais, kufuatia kifo cha marehemu Dk Omary Ali Juma.

“Rais Karume, Rais Mkapa wote wameniamini kwa dhati sana niitumike Zanzibar na niitumike Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Mkapa alinipa heshima kubwa sana. Nafasi ile sikuitara- jia, sikuiwaza, sikuilalia, sikuiamkia. Lakini kwa mapenzi yake akanipa wadhifa huo wa kumsaidia katika kazi zake, Mheshi- miwa Benjamin Mkapa nakushuru sana, nakushu- kuru kwa uamuzi wako huo,” alisema.

Vilevile, alimshukuru Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwa kumteua kuwa mgombea mwenza wake alipopende- keza jina lake kwenye Ka- mati Kuu ya CCM na kwa kauli moja Mkutano Mkuu ukaridhia awe mgom- bea mwenza na baadaye akawa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kwa hiyo nimetumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Makamu wa Rais kwa miaka tisa na miezi sita. Nimepata hes- hima kubwa, sio watu wote wa Zanzibar wanapata hes- hima kama hiyo, kwa hiyo namshukuru sana Mungu.

Lakini katika utumishi wangu huo, wa serikali hizi mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zan- zibar, ambao watu hawajui nataka nitamke waziwazi Mwenyezi Mungu ame- nijalia kuwa na miaka 72 na kidogo sasa, na miaka 51 nimekuwa mtumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Aidha, Dk Shein aliwaomba radhi wanaCCM, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kama kuna mahali aliteleza katika kutekeleza majukumu yake. “Nimetimiza wajibu wangu.

Pale nilipokosea naomba radhi kwa viongozi wenzangu, haikuwa nia yangu kukosea, nia yangu ilikuwa nifanye vizuri na niitumike nchi yangu vizuri. Miaka 10 iliyopita nilithibitishwa na Mkutano Mkuu niwe mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nimekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar kwa takribani miaka 10 kasoro miezi miwili ijayo. Kwangu ni heshima kubwa na nimesaidia na viongozi mbalimbali,” alisema.

Dk Shein alisema kazi ya urais, ameifanya kwa kiwango anachoona ni cha kutia moyo na ni kiwango kizuri, lakini akiwa mwa- nadamu mwenye mapun- gufu yake, yapo aliyofanya vizuri na yapo aliyoteleza na kukosea.

Hivyo, alisema anawaomba radhi wana- CCM wote, Wazanzibari wote na Watanzania wote. “Niwaambie wana- CCM wenzangu wa Unguja, tuna kazi kubwa sana kazi ya kukipa ush- indi chama chetu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambao kila chama na kila kiongozi anaweza na anadhamiria achagu- liwe yeye na chama chake, nasema CCM tunaendelea kushinda,” alisema.

Dk Shein alibainisha kuwa amekuwa akifanya kazi bega kwa bega na Rais John Magufuli na kusisitiza kuwa hakuna miongoni mwao, ambaye amemtilia shaka mwenzake. “Tumeshirikiana na yeye (Rais Magufuli) katika kila hali, kila wakati, kila siku wiki, kila mwezi kwa miaka yote mitano, tumeshikamana kwa dhati, hakuna moja kati yetu mwenye walakini na mwenzake,” alisema.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi