loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dereva aliyetumbukiza basi lenye abiria Kitonga bondeni anaswa

J ESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Baraba- rani mkoa wa Iringa, limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la Prez- dar, Said Abas Said (30) aliyesababisha ajali katika mlima Kitonga wilayani Kilolo hivi karibuni na kuua watu 10 na kujeruhi 36. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire jana kuwa dereva huyo alifani- kiwa kukimbia baada ya ajali hiyo.

“Amekamatwa juzi katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya akiwa amejificha kwa baba yake mdogo,”alisema. Kamanda alisema kuwa Juni 27 wakati dereva huyo, akiendesha basi hilo lenye namba za usajili T 326 CSX aina ya Yutong linal- oitwa Prezdar, alisababisha ajali hiyo akiwa safarini kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam na kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.

Kamanda Bwire alisema kuwa basi hilo, liliacha njia katika mlima Kitonga na kutumbukia bondeni kwa uzembe wa dereva huyo. Alisema kuwa mmiliki wa basi hilo, Neechi Msuya (40) mkazi wa Dar es Salaam, alijisalimisha kituoni Juni 30 mwaka huu, am- balo alitakiwa asaidie kumtafuta dereva huyo.

Alisema kuwa dereva huyo atafikishwa mahakamani ili mkono wa sheria uweze kuchukua mkondo wake. Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Yusuph Kamota aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza au kumaliza ajali.

Alisema kuwa madereva wanatakiwa kutii sheria bila shuruti, ikiwemo kujisalimisha ndani ya saa 12 wanaposababisha ajali, kwa kuzingatia kifungu cha sheria za usalama barabarani namba 57.

Kamota alisema kuwa mtu yoyote ambaye ni dereva asipojisalimisha ndani ya saa 12 zilizotolewa kisheria, atakamatwa tu, kwani jeshi lina mkono mrefu na macho makali ku- weza kubaini wanaokimbia, kama ambavyo wameweza kumkamata dereva huyo wa basi la Prezdar.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Na Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi