loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walima mwani Mchinga watakiwa kuunda ushirika

WADAU wa kili- mo cha mwani wa Kata ya Mchinga mkoani Lindi, wametakiwa kuunda ush- irika ili kuweza kupata misaada mbalimbali, iki- wamo ya elimu na fedha za kutanua kilimo chao. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Lango mkoani Lindi, Michael Mwanga.

Akizungumza katika utoaji wa elimu, kwa wananchi wa kata hiyo kuhusu kilimo cha mwani, alisema ili kusukuma mbele kilimo hicho wananchi wanat- akiwa kuungana na kuwa na ushirika.

Alisema kutokana na haja hiyo, wamemua kusaidia elimu kwa wananchi hao kupitia mradi wa kup- inga ukatili wa kijinsia na kuwezesha wanawake na vijana kliuchumi. Mwanga alisema pamoja na kupeleka elimu hiyo katika kata Mchinga kwenye vijiji vya Mchinga 1, 2 na Ruvu, pia watapeleka vifaa vya kilimo cha mwani, kwa lengo la kuongeza tija miongoni mwa wakulima wa mwani.

Alisema kupitia mradi huo, wakulima na wata- alamu watapata nafasi ya kujadiliana namna ya kuboresha uzalishaji wa zao la mwani katika Kata ya Mchinga iliyopo Manispaa ya Lindi.

Mwanga alisema kwamba shirika hilo kwa ufadhili wa shirika la Oxfam Tanza- nia, litawapatia nyenzo za kazi wakulima hao, ikiwamo kamba na viatu vya chacha na kuwasaidia kupata elimu muafaka wa zao hilo.

Zao la mwani linalolimwa kandoni mwa bahari, limekuwa likidorora mwaka hadi mwaka kutokana na uzalishaji usiokuwa na tija. Wakulima wa mwani walishukuru kuwapo kwa mradi huo, wakiamini kwamba utawasaidia kuongeza maarifa katika uzalishaji.

Mohamed Mikidadi kutoka Kijiji cha Mchinga 1 alisema kutokana na faida ya mwani, kitendo cha Lango kuwapatia elimu, kitabore- sha kilimo chao na kuwa na tija kubwa.

Aliitaka serikali kusaidia kilimo hicho chenye faida kubwa, kwa kuwa mali ghafi ya kutengeneza sabuni, dawa za mswaki, chakula. Alisema kwa kusaidiwa elimu ya ushirika na wao kuanza kujipanga, watazalisha zaidi kwani wana uwezo wa kuzalisha tani 1.5 wa mwani.

Hawa Kihinga alisema kwamba wanakubaliana na wazo la kuwapo kwa ushirika, kwani faida yake iko wazi. Shaha Hussein alisema amefurahishwa na elimu ya ushirika na kwamba wanataka kuingia ili kuondoa kero.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mchinga 1, Salum Seif alisema pamoja na kuwashukuru Lango, hatua zilizochukuliwa na wakulima katika ushirika na elimu ni za kuungwa mkono.

Alisema wao kama serikali wapo tayari kushirikiana na Lango kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuchukua hatua inapoona ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalumu, Lindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi