loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tasaf yaanza ‘safishasafisha’

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara mbili mfululizo fedha za wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini, unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), zitaondolewa kwenye mpango huo kwa kuwa zitakuwa zimekosa sifa.

Ofisa Malipo Kwa njia ya Mtandao wa Tasaf, Zacharia Nyinyimbe alibainisha hayo kwenye kikao kazi kwa wakuu wa idara na vitengo pamoja na mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya Tasaf na zoezi la uhakiki wa walengwa wa kaya masikini.

Pia, Nyinyimbe alisema kaya zilizo na washiriki waliopata uongozi, ikiwemo wenyeviti wa mitaa au vitongoji, zitakumbwa na ‘safishasafisha’ hiyo kwa kuwa zitakuwa zimepo- teza sifa ya kunufaika na mpango huo.

Alisema hatua ya kuziondoa kaya zenye mwonekano huo ni kuondoa migongano ya kimaslahi, kwa kuwa upo uweze- kano mkubwa kwa baadhi ya viongozi, kutumia nafasi zao kunufaisha kaya zao na kuzua manung’uniko ndani ya jamii.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo mengi ...

foto
Mwandishi: Na Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi