loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ikulu Chamwino yafunika nchi za Afrika Mashariki

TAKWIMU za kihistoria za Ikulu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaonesha kuwa Ikulu ya Chamwino nchini Tanzania ndiyo kubwa kwa eneo kuliko nchi yoyote katika kanda hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi, Ikulu ya Chamwino ina eneo la ekari 8,473 likiwa ni eneo kubwa kuwahi kuonekana katika makazi ya Mkuu wa nchi nchini Tanzania kwani malengo ya Mwalimu Julius Nyerere awali yalikuwa ni kuwa na eneo la ekari 61 tu.

Ukubwa huo kwa wa eneo la Ikulu ya Chamwino umeifanya Tanzania kuongoza kwa kuwa na eneo kubwa na lenye wanyama wengi kuliko nchi nyingine yoyote katika nchi za Afrika Mashariki.

Kulingana na historia za Ikulu za nchi mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizowekwa katika tovuti ya Ikulu, Kenya ndiyo ya pili kwa kuwa na eneo kubwa la Ikulu ya Nairobi ambalo lina ukubwa wa ekari 740.

Hii maana yake ni kwamba eneo la Ikulu ya Nairobi linaingia katika eneo la Ikulu ya Chamwino mara 11.5. Kimahesabu kunapatikana uwiano kati ya ukubwa wa Tanzania ikilinganishwa na nchi zingine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikulu ya Entebbe nchini Uganda inashika nafasi ya tatu kwa ukubwa wa eneo katika nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 1,747,200 ambalo ni sawa na ekari 430.

Kwa ukubwa huu ni dhahiri kuwa Ikulu ya Entebbe itaingia mara 19.7 katika Ikulu ya Chamwino hali inayoifanya Chamwino kuwa ikulu bora kuliko zote Afrika Mashariki.

Mbali na ukubwa, kuna wanyama waliopo katika eneo hilo karibu kila nchi, lakini kwa Tanzania hali imekuwa tofauti kutokana na kuwa na wanyama wengi kiasi kwamba inakuwa kama hifadhi ndogo.

Kingine kikubwa ni kuwa Ikulu ya Chamwino ni nyumbani kwa wanyama mbalimbali ambapo aina ya wanyama na idadi kwenye mabano ni pundamilia(120), swala(210), twiga(16), Kubu(36), batamaji(100), pofu(40), tausi(520), digidigi( 340), sungura pori (460), kanga pori (300) na ndege 24.

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi