loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bilioni 2/- zatumika miradi Tarime

SERIKALI ya Awamu ya Tano imepeleka Sh bilioni 2,128 katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kugharamia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu kwenye taasisi za kijamii.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa alisema mjini Tarime kuwa fedha hizo zitagharamikia ujenzi wa nyumba za walimu, mabweni, vyumba vya madarasa na kukarabati mifumo ya maji na umeme.

Alisema Sh milioni 968.7 zitatumika kukarabati miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Tarime na Hospitali ya Mji huo ambayo inayohudumia wananchi wengi kutoka vijijini na wilaya jirani ya Rorya.

“Shilingi milioni 400 zimeelekezwa katika ujenzi wa nyumba tatu za watumishi na ukarabati wa mfumo wa maji katika hospitali hiyo ili kuwawezesha wahudumu wa afya na madaktari kuishi karibu na maeneo ya utoaji huduma kwa wananchi wanaofika kutafuta huduma za kitabibu,” alisema Ntiruhungwa.

Alisema Halmashauri hiyo pia inatarajia kujenga vyumba 16 vya madarasa, kununua madawati 240 na kujenga matundu 46 ya vyoo katika shule mbalimbali katika eneo lote la mji wa Tarime.

Mkurugenzi huyo alisema kupitia wakala wa barabara vijijini na mjini Tarura usanifu unaendelea wa maandalizi ya ujenzi wa barabara inayozunguka soko kuu pamoja na kipande cha barabara kiwango cha lami eneo la uwanja wa michezo wa Serengeti.

“Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kutuletea fedha hizo ambazo zitatumika kutekeleza miradi mingi na hivyo kuongeza kasi ya kuhudumia wananchi na hivyo kuwapunguzia gharama za maisha ya kila siku,” alisema.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Tarime

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...