loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jumuiya za kidini zaonywa nyumba za ibada

SERIKALI imezionya jumuiya za kidini kutoruhusu nyumba za ibada kutumika kama majukwaa ya kisiasa au kushabikia mgombea yeyote katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Ukuu wa Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani Oktoba mwaka huu.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Simbachawene alisema wa kuwa mchakato wa uchaguzi mkuu umeshaanza ikiwemo teuzi za wagombea ndani ya vyama vya siasa na hatimaye uchaguzi, wizara yake inazikumbusha jumuiya hizo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na malengo waliojiwekea katika katiba zao.

Alizionya jumuiya zote za kidini na kijamii kutoshiriki au kushabikia chama chochote cha siasa au mgombea yeyote kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pia imezitaka jumuiya zote na wananchi kutojihusisha na vitendo vya kutoa kauli zinazoashiria au kusababisha chuki au kuamsha hisia za chuki miongoni mwa jamii, bali watumie haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni bila kuvunja sheria za nchi.

Waziri Simbachawene alisisitiza kuwa jumuiya yoyote iwe imesajiliwa au haijasajiliwa itakayokiuka sheria za nchi na kufanya vitendo au kutoa kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani au kuchochea chuki kwa kisingizio cha uhuru wa mawazo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya jumuiya, kikundi au mtu atakayetenda kosa hilo.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...