loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NEC tayari kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema iko tayari kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani Oktoba mwaka huu kwa kuwa mambo yote ya msingi likiwemo daftari la wapiga kura yameshakamilika.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dk Wilson Mahera (pichanin) wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds.

Dk Mahera alisema uboreshaji wa daftari la wapiga kura unakwenda vizuri na litakuwa tayari ndani ya wiki moja kuanzia sasa. Alisema watu wameshahakiki taarifa zao, tume imeshapokea baadhi ya vifaa vitakavyotumika kutolea mafunzo na wameshaanza kuvisambaza kwenda kwenye halmashauri 184 ili halmashauri hizo nazo zisambaze kwenda kwenye kata 3,956 na hatimaye visambazwe kwenye ngazi za chini.

“Kwa hiyo tumeanza, tunaendelea na tunasubiria kwa ari kubwa tarehe ile ya gazeti la Serikali ambalo wakati wowote kuanzia sasa hivi linaweza likatoka na litakapotoka, hatua inayofuatia ni uteuzi na kuratibu kampeni nchi nzima, vyama vitaleta ratiba zao,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk Charles, baada ya kuratibu kampeni, wataanza kusafirisha vifaa kwenda sehemu mbalimbali za nchi. Alisema tangazo la kuvunjwa kwa Bunge litakapotoka kwenye gazeti la Serikali ndipo Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapopanga tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kuhusu majimbo ya uchaguzi, alisema yatakuwa majimbo 214 kwa upande wa Tanzania Bara na majimbo 50 upande wa Tanzania Zanzibar na majina ya majimbo hayo yatatangazwa hivi karibuni pamoja na kata 3,956.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara idadi ya majimbo ilikuwa hiyo hiyo 214 na upande wa Zanzibar yalikuwa 54, lakini kwa sasa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeyapunguza kutoka majimbo 54 hadi 50, hivyo kufanya jumla ya majimbo yote bara na visiwani kuwa 264.

“Kwenye uchaguzi mkuu ujao tutakuwa na vituo zaidi ya 75,000 vya kupigia kura na kila kituo kitakuwa na watu watano akiwemo msimamizi wa kituo cha kupigia kura akisaidiwa na wasimamizi wawili, karani pamoja na mlinzi,” alisema.

Pasipo kutaja idadi, Mkurugenzi huyo alisema mwaka huu vijana walijiandikisha kwa wingi na kuwataka wajitokeze kwa wingi pia wakati wa kupiga kura ili wawachague viongozi watakaolinda maslahi yao.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 4 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...