loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mrema ataja mikakati ya uchaguzi TLP

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema chama hicho kitasimamisha wagombea ubunge wanne katika majimbo ya Arusha, Moshi Vijijini, Mwanga pamoja na Kyela huku madiwani wanane nao wakiwania nafasi hiyo katika Jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa wakati akipokea wanachama wapya, Mrema alisema kuwa wanaosema TLP imenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapoteza muda kwani chama hicho kimeamua kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa sababu ya utendaji kazi, huku kero mbalimbali za wananchi zikiwa zimetatuliwa.

Alisema TLP si wajinga pale waliposema wanamuunga mkono Rais Magufuli kwani wanajua wanafanya siasa za kistaarabu na si siasa zenye kutukana au kubeza mtawala aliyepo madarakani pasipo kuwa na hoja za mashiko.

Alisema chama hicho kimeamua kusimamisha wagombea hao wa ubunge na udiwani kwani wanaamini kuwa wanapata wawakilishi wengi katika kila halmashauri pamoja na wabunge watakaotokana na chama hicho.

“Sasa mimi kama mwenyekiti naanzaje kumpinga mtu ambaye alipokuja kwenye jimbo langu kipindi kile nikiwa mbunge aliwaambia wananchi waniunge mkono na wananchi walikubali kunichagua, je leo mimi ni nani nisimuunge mkono tena si maamuzi yangu ni ya wanachama wa TLP, mimi kunichagua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole na nitaongoza hadi mwaka 2023, jamani kwa nini iwe mimi, kwani wengine hawapo? Mjue nina akili zangu,”alisema.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...