loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchakato wa kununua meli mpya Ziwa Tanganyika waanza

KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho amesema mchakato wa kununua meli mpya ya mizigo katika Ziwa Tanganyika umeshaanza.

Alitoa kauli hiyo alipozungumza na Habari- LEO jana lililotaka kujua kama ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa ya kununua meli mpya katika ziwa hilo wakati akivunja Bunge Juni 16 mwaka huu jijini Dodoma imeanza kufanyiwa kazi.

Dk Chamuriho alisema hatua ambayo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeanza nayo na inaendelea kwa sasa ni kuandaa andiko la mradi huo.

Alisema kipindi hiki cha Julai ni cha mipango kuhusu mchakato wa kununua meli hiyo na andiko hilo la mradi litakamilika katikati ya mwezi ujao. Dk Chamuriho alisema kukamilika kwa andiko hilo kutatoa fursa kwa hatua zingine kufuata, ikiwemo kutangaza zabuni pamoja na kujua ukubwa na uwezo wa meli hiyo.

Wakati akivunja Bunge, Rais Magufuli alisema meli hiyo mpya itakuwa ikifanya safari zake kati ya Bandari ya Kalema kwa upande wa Tanzania na Bandari ya Kalemie kwa upande wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Magufuli alisema kukamilika kwa meli hiyo kutafanya mizigo inayotoka katika bandari za Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam kutopita tena katika nchi za jirani, badala yake itakwenda moja kwa moja hadi Bandari ya Kalema na hatimaye DRC.

Alisema lengo ni kuhakikisha Tanzania inajenga uchumi mkubwa kwa kuunganisha shughuli za kibiashara na DRC kupitia meli hiyo. Sambamba na hilo, Rais Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itanunua meli mpya itakayokuwa inatoa huduma kati ya Bandari ya Mtwara na Visiwa vya Comoro.

Katika kuboresha usafiri kwa njia ya maji, Serikali ya Awamu ya Tano imefanya upanuzi wa Bandari Kuu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga pamoja na kuboresha usafiri katika Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa na kuziboresha bandari za maziwa hayo.

Katika Ziwa Victoria, aerikali imenunua meli mpya kubwa ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu inayoendelea kujengwa katika Ziwa hilo na itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, pia imekarabati meli zilizopo katika Ziwa hilo ikiwemo Mv Victoria, Mv Butiama, Mv Umoja na Mv Clarias.

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika, mbali na mipango ya kununua meli mpya, Serikali ya Magufuli pia imekarabati meli ya mafuta ya Mt Sangara na mipango ya kuikarabati meli ya Mv Liemba nayo inaendelea.

Kwenye Ziwa Nyasa, serikali imenunua meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo, huku Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) chini ya Rais Dk Ali Mohamed Shein ikinunua meli kubwa mpya mbili kwa ajili ya kutoa huduma kwenye Bahari ya Hindi.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...