loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kibaha waanzisha madarasa ya wajawazito

IDARA ya Afya ya Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani imeanzisha madarasa ya wajawazito wenye upungufu mkubwa wa damu kupunguza vifo vya akinamama wakijifungua.

Mratibu wa huduma ya uzazi, Prisca Nyambo alisema hayo wakati wa mafunzo ya namna ya matumizi ya vyakula vinavyoongeza damu. Alisema changamoto inayosababisha vifo vya wajawazito ni upungufu wa damu tangu mama anapopata ujauzito na kusababisha hatari.

“Tunatoa mafunzo kwa makundi ya wajawazito wenye upungufu mkubwa wa damu kuanzia gramu tisa walio katika hatari na tunawafuatilia hadi wawe na hali nzuri vifo vingi hutokana na upungufu wa damu,” alisema.

Alisema wajawazito hao wameonesha hatari baada ya kuanza kliniki ambao wanafundishwa namna ya kula na kuandaa vyakula ambavyo vinaongeza damu na wanapaswa kujua athari za upungufu wa damu kabla ya kujifungua.

“Tatizo siyo uwezo kununua vyakula ambavyo vinaongeza damu na kuna dhana labda mtu ale nyama ndiyo inasaidia lakini kuna vyakula vya bei nafuu na vinapatikana kwa urahisi,” alisema.

Alisema wanatoa mafunzo kwa wahudumu wa majumbani ili wakiona mjamzito ana dalili mbaya wachukua hatua kwani tatizo akinamama hao wanakuwa na uzito kuchukua maamuzi ya kwenda hospitali wanapoona dalili mbaya.

Ofisa lishe wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Salma Mohamed alisema kikubwa walichokuwa wanawaelekeza ni maandalizi ya chakula hasa mboga zinazoongeza damu pamoja na viungo.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...