loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yatoa milioni 226/- Halmashauri ya Nyasa

SERIKALI imetoa Sh milioni 226 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kutekeleza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na matundu ya vyoo 17 katika shule ya msingi Ukuli Kata ya Kingerikiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Jimson Mhagama alisema serikali imetoa Sh milioni 200 kujenga jengo hilo na matundu sita ya vyoo Kituo cha Afya Kingerikiti.

Alisema mradi huo ulianza kutekelezwa Aprili 24 mwaka huu na unatarajia kukamilika Agosti 30 mwaka huu ambapo mradi upo hatua ya jamvi ukiwa na asilimia 25 na hatua ya renta ni asilimia 47 na unatekelezwa kwa force account.

Eneo la mradi lina ukubwa wa ekari 18, hadi sasa mradi umetoa ajira za muda kwa watu 30 na unatekelezwa kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Kingerikiti kutoka vijiji vinne vya Kingerikiti,Ukuli, Lumecha na Mawasiliano.

Akizungumzia mradi wa matundu 17 ya vyoo shule ya msingi Ukuli, Mkurugenzi huyo alisema serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 26 kupitia fedha za udhamini kutoka SWASH kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo.

Alisema utekelezaji wa mradi huo umeanza Juni 3 na ulipangwa ukamilike Juni 30 mwaka huu. Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Nuru Ngeleja amewapongeza wananchi wa kijiji cha Ukulu kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya vyoo ili wanafunzi wa shule hiyo wawe na mazingira rafiki kusoma na kulinda afya zao.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Nyasa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi