loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polisi wafundisha waendesha bodaboda 20,000

WAENDESHA bodaboda 20,000 wamenufaika na mafunzo ya Kikosi cha Matengenezo ya Magari ya Polisi kuhusu sheria na kanuni za usalama barabarani na matumizi ya barabara.

Konstebo wa Polisi, Jackson Manifred alisema kwa miaka miwili wamekuwa wanawafuata waendesha bodaboda 25 katika vituo vyao na kuwapa elimu hiyo hali iliyoongeza uelewa wao kuhusu sheria na matumizi sahihi ya barabara. Alikuwa akizungumza katika banda la Polisi kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika hivi karibuni Viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Alisema walibaini wapo watu wengi wanaojua kuendesha pikipiki, lakini hawajui sheria na kanuni za usalama barabarani na matumizi sahihi ya barabara hali inayochangia ajali.

“Tuligundua ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wasio na elimu hii wakiwamo wa magari madogo binafsi ambao hawajui sheria za usalama hivyo wanasababisha ajali kwa bodaboda hata kwa wao wenyewe,” alisema.

Akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo, alisema waendesha bodaboda wengi wakiwamo wanawake wamenufaika na elimu hiyo inayohusisha pia ujasiriamali ili kazi ya bodaboda iwaletee faida na kuwafanya wajitegemee na kuitumia kama kazi nyingine.

“Katika kikosi pia tunafundisha madereva wa pikipiki kwa kuanzia uelewa wa sehemu na mambo muhimu ya pikipiki kwa wiki sita au zaidi kutegemea wepesi wa uelewa wa mwanafunzi na kuwatafutia leseni,” alisema.

“Wahalifu wengi ni vijana wasio na shughuli maalumu, hivyo lazima wapunguzwe kwa kuwa na shughuli halali za kufanya ili wawe na kazi ya kuwaingizia kipato halali,” alisema.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...