loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kusaya aagiza wasiolipa ada chuo wasifukuzwe

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ameagiza uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo na Mifugo (MAMRE) cha Wanging’ombe mkoani Njombe kutowafukuza wanafunzi wasiolipa ada ya mafunzo.

Kusaya ametoa agizo hilo juzi alipofanya ziara kukagua maendeleo ya chuo na kuzungumza na wanafunzi. Alisema uongozi wa chuo utafute njia rafiki kusaidia wanafunzi wenye mazingira magumu yanayofanya wasilipe ada mapema.

“Vyuo vyote 29 (14 vya serikali na 15 vya binafsi) ni vyangu kwani vinalenga kuzalisha maafisa ugani watakaoenda kuhudumia wakulima. Nitaendelela kuvisaidia bila kuangalia nani anakimiliki muhimu vitoe mafunzo bora kwa wanafunzi,” alisema.

Katibu Mkuu huyo aliahidi kutoa kompyuta ili kuwezesha kuanzisha maktaba mtandao na kugharimia mwanafunzi mmoja kwenda kujifunza kanuni bora za ufugaji kuku kisasa chuo cha Ihemi Iringa kwa gharama za serikali.

Alisema ili kuboresha mafunzo kwa vitendo atakipatia chuo hicho Kitalu nyumba kifundishe kilimo cha mbogamboga na matunda pia. Chuo cha MAMRE kina wanafunzi 103 wa ngazi ya astashahada na stashahada.

Kaimu Mkuu wa chuo, Geoffrey Mapesa alisema changamoto ni kukosa mfumo wa udahili wa pamoja na kusababisha upungufu wa wanafunzi. Wanafunzi 169 wamehitimu mafunzo ya kilimo na mifugo tangu chuo kilipoanzishwa mwaka 2014 chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Njombe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...