loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waganga tiba mbadala, asili kupewa vibali

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora imetoa siku 21 kwa waganga wote wa tiba asilia na tiba mbadala wilayani humo kuwa na vibali maalumu vitakavyowatambulisha.

Agizo hilo liLItolewa jana na Ofisa Utamaduni wa halmashauri ya wilaya hiyo, Marko Kapela alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria hafla ya kuwaaga waganga 24 waliohitimu mafunzo ya utoaji tiba asilia na tiba mbadala kijiji cha Kagera, kata ya Kashishi.

Alisema waganga wamekuwa wakifanya shughuli hizo kiujanja ujanja pasipo kufuata taratibu hali ambayo imekuwa ikisababisha kukamatwa na kufikishwa vyombo vya sheria.

Alisema ili kuepuka usumbufu wanaopata sasa kila mtu anapaswa kukata kibali cha kufanya shughuli hizo kwa uhuru na mahali popote.

Alisema serikali inajua mchango wa waganga wa tiba asilia na tiba mbadala kuhudumia wananchi, ndiyo maana iliweka utaratibu mzuri wa kuwasajili watambulike na kutobughudhiwa.

Alisema Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliweka utaratibu pia waganga wa kujisajili Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala ili wapeane zoefu wa kazi zao.

Msimamizi Mkuu wa Mafunzo hayo, Kulwa Ndomelo alisema hadi sasa wananchi 71 wa Tabora, Kigoma, Shinyanga, Geita, Katavi, Mwanza, Rukwa na Simiyu wamehitimu mafunzo tangu aanze huduma mwaka 2013.

Alisema mafunzo hayo ni ya aina yake kwani wanafunzi hufundishwa namna ya kutumia miti, mimea na udongo kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii na tiba hiyo huwa haihusiani na ushirikina wala ramli chonganishi.

Alisema huduma hiyo iliyopewa jina la ‘Tiba ya Msalaba’ inafanywa kwa imani ya Mwenyezi Mungu na wanaofundishwa hawaruhusiwi kujihusisha ushirikina wala ramli chonganishi. Aidha alisema mafunzo hayo yanatolewa bure kwa miezi sita ambapo wahitimu huagwa ili warudi kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi