loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki Stanbic Tanzania yaeleza siri mafanikio

BENKI ya Stanbic Tanzania imesema siri ya kukua kibiashara imetokana na maendeleo ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo nchini, Kevin Wingfield (pichani) alisema hatua hiyo imewapa motisha ya kuunda kauli mbiu mpya ya ‘Inawezekana’ ambayo inafanana na nafasi yake katika jamii.

“Tukiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini, tumefanya tathmini na kugundua maendeleo ya benki yetu katika kukua kibiashara yamechagizwa na maendeleo ya wateja wetu na wananchi. Hivyo tukachochewa kuja na kauli mbiu inayokwenda sambamba na ukuaji wa benki yetu,”alisema.

Alisema kaulimbibu hiyo inaakisi benki hiyo imekua, inavyoendelea kukua kutokana na huduma bora wanazotoa kwa wateja na mtazamo wa wateja wao na fursa zilizopo.

Alisema benki yake inaamini ndoto ni chachu ya maendeleo, hivyo ni lazima benki hiyo na wateja wake kwa pamoja kuwa tayari kuchukua hatua mpya ili kufanikisha ndoto zao hizo.

“Tulipounda kauli mbiu hii, tafiti zilionesha watu na biashara zao, hutafuta mtoa huduma anayewaamini na anawahamasisha. Wanahitaji benki itakayowawezesha kufikia malengo yao binafsi na kibiashara na ambayo itawathamini katika kila jambo. Kauli mbiu ya ‘Inawezekana’ inatupa fursa kufanya hivyo,”alisema.

Aidha, alisema mwelekeo huo mpya ni kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuhusu Tanzania ya kesho wakionesha ubunifu wa suluhu ambazo zinalenga kutoa huduma fanisi kwa wateja wao.

MBUNGE wa Mbeya mjini Dk Tulia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi