loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZAECA yatakiwa kukomesha rushwa

MAMLAKA ya Kupambana na Rushwa Zanzibar (ZAECA), imetakiwa kupambana na vitendo vya rushwa, kwa kuangalia matukio hayo kwa vyama vya siasa ikiwemo vya upinzani.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mjini Magharibi, Mgeni Mussa Haji alisema moja ya vipaumbele vya chama hicho ni kuhakikisha matukio ya kupambana na rushwa, yanatokomezwa moja kwa moja.

Alisema rushwa haina nafasi katika CCM na ndiyo maana watendaji wa Zaeca, wamekaribishwa kuja kutoa mada juu ya mikakati ya kupambana na rushwa na athari zake kwa vyama vya siasa.

Hata hivyo, Haji aliwataka watendaji wa mamlaka hiyo, kuhakikisha wanafika kwa viongozi wa vyama ya siasa ikiwemo vya upinzani na kutoa elimu, ikiwemo kuratibu uchaguzi na uchukuaji fomu.

‘’Viongozi wote wa CCM ikiwemo na wanachama wake wanafahamu madhara ya rushwa kutokana na elimu inayotolewa na Zaeca, tunataka shughuli hii iende kwa wenzetu wa vyama vya siasa vya upinzani ili kufikia malengo ya kutokomeza rushwa katika siasa na uchaguzi,’’alisema.

Ofisa kutoka Zaeca, Saada Salum alisema wamejipanga vizuri, kuhakikisha wanayafikia makundi yote muhimu ya vyama vya siasa ikiwemo vya upinzani.

Alisema rushwa ni adui wa haki, ambapo katika uchaguzi mbalimbali wagombea huitumia kwa ajili ya kutekeleza matakwa yao, ikiwemo kugombea nafasi za juu za uongozi.

‘’Sheria ya Mamlaka ya Kupambana na Rushwa haifanyi kazi kwa Chama Cha Mapinduzi tu, inavihusu vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa,’’alisema.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi