loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

…Wavunja kambi, wamuunga mkono Dk Mwinyi

WAGOMBEA 32 waliowania urais wa Zanzibar, wametamka rasmi kuvunja kambi zao na kuunganisha nguvu kwa mgombea aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Dk Hussein Mwinyi.

Wamesisitiza kuwa watahakikisha CCM, inaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Mmoja wao, Pereira Ame Silima alisema ugombea wao sasa umekwisha na makundi yote yanatakiwa kuunga nguvu zao kwa Dk Mwinyi.

Silima alisema mgombea aliyeteuliwa na CCM, anatosha kupeperusha bendera ya chama na ataleta ushindi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba. ‘’Nipo hapa kumpokea mgombea wa CCM kwa sababu nimevunja kambi yangu.

Sisi wagombea 32 tulioshiriki katika mchakato wa awali wa kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar, sasa tunavunja kambi zetu na kuelekeza nguvu kwa chama chetu,’’alisema Silima.

Aidha, Ayoub Mohamed aliwataka watu waliokuwa wakimuunga mkono, kuhamisha nguvu zao kwa mgombea aliyeteuliwa na CCM, Dk Mwinyi.

Alisema wajumbe wa NEC ya CCM, hawakufanya makosa walipomchagua Dk Mwinyi kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kwani wana imani kubwa ataendeleza mazuri yote yaliyoasiwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Mgeni Hassan Juma ambaye ni miongoni mwa wanawake watano waliochukua fomu hizo kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, alisema mgombea aliyeteuliwa na NEC na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, anatosha kuiletea ushindi CCM, kutokana na kubeba historia na sifa zilizotukuka katika utumishi wake katika serikali zote mbili.

Juma alisema kuwa ana matarajio makubwa kwamba katika kipindi chake cha uongozi, Dk Mwinyi atatoa kipaumbele kwa wanawake na masuala ya kijinsia. Alisema kuwa anataka kuona mwanamke, anapata nafasi kubwa ya kushiriki katika nafasi za uongozi.

‘’Sina matatizo kabisa na mgombea wetu ambaye tumemkabidhi usukani kulivusha jahazi letu katika safari ya uchaguzi mkuu, matarajio yetu masuala ya usawa wa kijinsia na wanawake na uongozi yatazingatiwa katika kipindi chake,’’alisema.

Aidha, Waziri wa Uwezeshaji, Wanawake na Watoto, Maudline Castico alisema kuwa amejenga matumaini makubwa kwa mgombea wa CCM, Dk Mwinyi kwamba ndiye chaguo la Wazanzibari katika mbio za urais.

‘’Sina mashaka na uwezo wa Dk Mwinyi katika kuongoza visiwa vya Unguja na Pemba, amepikwa siku nyingi na sasa yupo tayari kuongoza,’’alisema.

Wagombea hao wa urais wa Zanzibar , walishiriki mapokezi ya Dk Mwinyi jana kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume hadi makao makuu ya CCM Kisiwandui wakiwa na wanachama wengine.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...