loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Vijana haswa miaka ya 1982 hawaridhiki

 

Rais Dk John Pombe Magufuli amesema kuwa vijana wengi ambao wamezaliwa miaka ya 1982, hawaridhiki na nafasi walizonazo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Julai 16, 2020 akiwa Ikulu ya Chamwino, Dodoma, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaapisha viongozi aliowateua, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Manyara,  Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya mbalimbali hapa nchini.

"Hii kazi umeipata kwa sababu Mungu alitaka, mkamtangulize Mungu katika kazi zenu lakini pia mkawatumikie wananchi maskini katika maeneo yenu, nipende kusisitiza kwamba katika kazi hizi, kuridhika ni jambo muhimu sana, unajua vijana saa nyingine hawaridhiki harakaharaka haswa waliozaliwa miaka ya 1982" amesema Rais Magufuli.

"Watu jifunzeni kuridhika, Selemani Serera (DC mpya Kongwa), ni PHD holder, lakini aliridhika na mshahara wake wa Sh. 500,000 pale CCM Makao Makuu, Sasa vijana waliozaliwa hasa miaka ya 82 hawaridhiki,” amesema Rais Dk John Magufuli mapema leo Ikulu, Dodoma wakati akiwaapisha viongozi wa nafasi mbalimbali za kiutawala Serikalini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu alisema, "Mwanadamu unapoishi lazima utosheke na kile ulichonacho, unapokuwa hutosheki na unahaha huku na kule Mungu ana maamuzi yake pia...

"...nendeni mkafanye kazi, mtumikie wananchi," amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Mungano wa Tanzania

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...