loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCM yakusanya zaidi ya Sh milioni 800 fomu za ubunge

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge au uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)inapatikana kwa 100,000/- ni wazi kuwa chama hicho pekee tayari kimeshakusanya zaidi ya Shilingi milioni 800 tangu ilipotangaza kufungua mchakato wa uchukuaji fomu nchi nzima.

Hadi jana (Agosti 15, 2020), jumla ya makada 8,205 walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuwania ubunge ndani ya chama hicho.

Akizungumza katika hafla ya kuwapisha Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurungezi leo Ikulu Chamwino Dodoma, Rais John Magufuli alisema mpaka jana jumla ya watia nia 8,205 walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu.

Alisema Dar es Salaam pekee hadi jana watia nia walikuwa wamefikia 829, Arusha 320, Kilimanjaro 82, Kagera 328.

 “Waliochukua fomu kuomba kuwania kwenye majimbo wapo 6,533, Viti Maalum 1,539, uwakilishi 133 jumla 8205, bado leo na kesho(ijumaa),” alisema Rais Magufuli.

Fomu za kuwania Ubunge au uwakilishi inapatika kwa Sh 100,000 kwa maana hiyo mpaka jana chama hicho kilikuwa kimevuna Sh 820, 500,000.

Hata hivyo, kwa idadi ya waliochukua fomu leo na watakaochukua kesho, ni wazi kuwa chama hicho kina uhakika wa kuvuna zaidi ya Sh bilioni moja kutokana na ada ya fomu.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa kesho ijumaa Julai 17 na kufuatiwa na mchujo kwa wagombea hao.

Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho zoezi la vikao vya kamati za siasa kuwajadili wagombea itaanza rasmi Agosti 4 na itahitimishwa Agosti 6, 2020 kwa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa kuwajadili wagombea na kufanya uteuzi wa mwisho.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humprey Polepole tayari ameweka bayana kuwa mchakato wa kupata majina ya wagombea utafanyika kwa njia ya uwazi na kuzingatia demokrasia.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

1 Comments

  • avatar
    Issa Kashingo
    17/07/2020

    Magufuli ameinua upendo ws siasa baada kazi nzito kuisafisha. Kila mtu leo anaamini kuwa siasa za maendeleo kama za Magufuli zinafurahisha na kuleta heshima.

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...